Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Salum Mwinyi Rehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Primary Question

MHE. SALUM MWINYI REHANI aliuliza:- Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Bwawa la Kidunda ambapo pia kutakuwa na miradi ya kilimo na ufugaji samaki. • Je, kuna tathmini ya kitaalamu iliyofanyika ya kudhtibiti kemikali zinazotokana na utumiaji mkubwa wa dawa za kudhibiti magugu kwenye mashamba ya miwa na mpunga na utumiaji wa mbolea za SA ambazo husababisha uharibifu wa ardhi? • Je, Serikali inaweza kuleta Bungeni ripoti ya tathmini pamoja na Environmental Impact Assessment juu ya mradi huo? • Je, mradi wa umwagiliaji utachukua ekari ngapi na imepanga kulima nini katika mashamba hayo?

Supplementary Question 1

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ningependa kumuuliza swali moja la nyongeza.
Kwanza, tunataka tupate ripoti na siyo cheti kwa sababu cheti kinakuwa ni uthibitisho tu, lakini ripoti ndiyo kitu ambacho tunaweza kuona athari iliyopo au hakuna athari.
Pili, nilitaka kuelewa kwamba bwawa lile liko maeneo ya upande wa Morogoro, lakini wananchi wa pale wanategemea sana kuzalisha pamoja na mazao ya miwa na mpunga lakini na mazao mengine mbalimbali ambayo yako katika eneo lile.
Je, wasiwasi wangu uliokuweko maporomoko ya maji na mwelekeo wa maji ambayo yanashuka katika lile bwawa hayatoweza kuathiri mmomonyoko na uharibu wa lile bwawa pengine labda ikasaidia kuingia na kufanya contamination ya maji ambayo yatakuwa yanaingia katika maeneo yale.
Je, Serikali iko tayari kuweka utaratibu mzuri wa kilimo ambacho kitakuwa hakitumii kemikali ili kuepukana na athari za kikemikali katika maji yale ambayo wanatumia binadamu na kilimo?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza ameomba kwamba kile cheti cha NEMC kiwasilishwe Bungeni, lakini kwa mujibu wa swali lake aliuliza, je, Serikali inaweza kuleta Bungeni ripoti ya tathmini pamoja na Environmental Impact Assessment juu ya mradi huo. Tumesema ndiyo tunaweza, sasa kama swali la pili unataka tulete basi utuagize tulete tutaleta, lakini kwa mujibu wa swali lako tumeshajibu kwamba tunaweza tukaleta.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kama ilivyojibiwa kwenye swali la msingi na Mheshimiwa Naibu Waziri ni kwamba ripoti ya NEMC ipo na imeweka tayari na Environmental Management Plan. Kwa hiyo, hakutakuwa na athari ya aina yoyote pale ambapo kutakuwa na athari basi ripoti ile itafuatwa wataweka utaratibu kuhakikisha kwamba madhara ya aina yoyote kuhusu kemikali hayatajitokeza, madhara kuhusu mmomonyoko pia hayatajitokeza. Kwa sababu utokaji wa maji kwenye bwawa utakuwa controlled kulingana na matumizi ya kupeleka maji kwenye mashamba pamoja na kupeleka maji Mto Ruvu.

Name

Omary Tebweta Mgumba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini Mashariki

Primary Question

MHE. SALUM MWINYI REHANI aliuliza:- Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Bwawa la Kidunda ambapo pia kutakuwa na miradi ya kilimo na ufugaji samaki. • Je, kuna tathmini ya kitaalamu iliyofanyika ya kudhtibiti kemikali zinazotokana na utumiaji mkubwa wa dawa za kudhibiti magugu kwenye mashamba ya miwa na mpunga na utumiaji wa mbolea za SA ambazo husababisha uharibifu wa ardhi? • Je, Serikali inaweza kuleta Bungeni ripoti ya tathmini pamoja na Environmental Impact Assessment juu ya mradi huo? • Je, mradi wa umwagiliaji utachukua ekari ngapi na imepanga kulima nini katika mashamba hayo?

Supplementary Question 2

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza kuhusu Bwawa la Kidunda.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri kwa sababu mradi huu mpaka sasa accessibility ya kufika sehemu ambayo inajengwa bwawa haifikiki kirahisi ni pamoja na utekelezaji huu, lakini kulikuwa na mpango wa kuiboresha na kuitengeneza barabara hii ili ujenzi huu uweze kuanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kujua katika upande wa Serikali, ni lini barabara hii itaanza kujengwa ili kurahisisha ujenzi wa bwawa huu kuanza?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mgumba kwa kuuliza swali ambalo ni la msingi, lakini jibu ni moja dogo kwamba katika mwaka wa fedha unaokuja tumetenga fedha, kwa hiyo utaiona hiyo fedha kwenye wasilisho la bajeti ya Waziri wa Maji ambapo tutaanza na ujenzi wa barabara ili kumwezesha Mkandarasi sasa awe na uwezo kwenda kujenga bwawa.