Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Primary Question

MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza:- Walimu Wilayani Maswa wana uhaba wa nyumba za kuishi; pamoja na juhudi za wananchi kujenga nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari lakini walimu hao bado wanahitaji kujenga nyumba zao wenyewe za kudumu. Je, ni lini Serikali itaweka utaratibu maalum wa kutoa mikopo kwa walimu hao ili wajenge nyumba zao binafsi?

Supplementary Question 1

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Spika, swali langu dogo tu la nyongeza ni kwamba kwa kuwa masharti ya mikopo kwenye mabenki na SACCOS nyingi ambazo kwa kweli watu wengi wamekopa na wameshindwa kulipa madeni na yamewasababishia umaskini mkubwa. Je, hamuoni kwamba kuna haja Serikali sasa mkatazama namna nyingine ya kuwapatia walimu hawa mikopo ya masharti nafuu ili waweze kujenga nyumba zao za kudumu? Swali la kwanza.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, mna mpango gani wa kuiwezesha Halmashauri ya Maswa kama tulivyoongea siku za nyuma, kwamba Halmashauri na zenyewe ziwe na uwezo au zijengewe uwezo wa kuchukua mikopo ili mikopo hiyo kupitia halmashauri iwasaidie walimu hao kujenga nyumba zao za bei nafuu? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, ni kweli mikopo mingine inayotokana na taasisi za benki ina changamoto nyingi sana, lakini kwa utaratibu wa sasa wa kuwasaidia wafanyakazi kuna suala la mortgage financing ambalo Bunge hili hili lilipitisha sheria humu ndani kuwawezesha watumishi mbalimbali waweze kupata fursa ya mikopo kupitia fedha wanazochangia katika mifuko yao ya Hifadhi ya Jamii.
Mheshimiwa Spika, katika hili naomba niwapongeze Utumishi Housing ambao wamefanya kazi kubwa sana katika maeneo mbalimbali hivi sasa. Tunaona wazi kwamba matangazo yao yametoka, sasa naomba tuwaambie watumishi wa Serikali, tutumie dirisha hili vizuri ili tuweze kupata nyumba katika maisha yetu.
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la kuziwezesha Halmashauri mbalimbali hasa Halmashauri ya Maswa, kupata mikopo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inafanya uwekezaji; kuhusiana na jambo hili mara nyingi sana ofisi yetu huwa inapokea vibali mbalimbali vya kutaka halmashauri kufanya uwekezaji katika eneo fulani. Hata hivyo mara nyingi sana ofisi yetu huwa inapitia haswa yale maombi kuangalia ili jambo likishapitishwa, likapatiwa kibali ambapo lisije likawa mzigo mkubwa sana kwa Halmashauri hiyo kiasi cha kushindwa kujiendesha.
Kwa hiyo, mawazo mazuri yanakaribishwa, na ofisi yetu ina wataalam watafanya analysis lile jambo linalofanyika basi Halmashauri hiyo haitawekwa nyuma kuhakikisha kwamba inapewa kibali ili ifanye uwekezaji katika halmashauri yake.