Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Martin Alexander Mtonda Msuha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. MARTIN M. MSUHA aliuliza:- Chama Kikuu cha Ushirika ‘Mbinga Cooperative Union (MBICU) kilishindwa kuendesha shughuli zake kibiashara na hatimaye kukabidhiwa kwa mfilisi mwaka 1994/1995 kutokana na madeni pamoja na kuyumba kwa soko la kahawa. (a) Je, kwa nini mfilisi bado anashikilia mali za Chama hicho badala ya kukabidhi kwa Chama kipya cha Mbinga Farmers Cooperation Union (MBIFACU) kwa muda mrefu kiasi hicho? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kulipa deni la wakulima lipatalo shilingi 424 millioni ambalo liliachwa na MBICU iliyokufa?

Supplementary Question 1

MHE. MARTIN M. MSUHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa mujibu wa majibu ya Serikali niliyonayo mezani jibu la Mheshimiwa Naibu Waziri halijakamilika bado part ‘B’. Ahsante.

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri itabidi nikutane na Mheshimiwa Msuha ili tuone ni kwa nini anafikiri swali langu au swali lake halijajibiwa vizuri. Kwa sababu sisi tulivyoliangalia tumejiridhisha kwamba alichotaka tumekijibu kwa sababu kimsingi aliuliza maswali mawili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza kwa nini Mfilisi bado anashikilia mali za chama hicho na tumejibu kwamba mfilisi hashikilii. Akauliza swali la pili, je, Serikali ina mpango gani wa kulipa deni la wakulima ambalo la shilingi milioni 424, hili nalo tumesema Serikali inaendelea kuangalia utaratibu wa kulipa. Kimsingi Serikali imeji-commit kwamba itaendelea kulipa. Sasa kama anaona bado halijajibiwa, nafikiri hakuna tatizo niko tayari kukutana naye, tujadiliane kwamba kwa nini anahisi bado halijajibiwa.