Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prosper Joseph Mbena

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. PROSPER J. MBENA aliuliza:- Ujenzi wa barabara kutoka Bigwa - Kisaki iko kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli alitoa ahadi ya kujenga barabara hiyo alipohutubia wananchi wa Morogoro na kwamba fedha za ujenzi zitatoka Serikalini, nyumba zote zilizomo ndani ya mita 60 zimewekwa alama ya ‘X’ tayari kubomolewa katika maeneo ya Ruvu Kibangile, Kisemu, Mtamba, Nzasa, Kangazi, Kisanzala, Tambuu, Mvuha, Mngazi hadi Kisaki:- • Je, Serikali itakuwa tayari kuwawekea wananchi hao utaratibu wa kuwajengea nyumba bora kwa wanaopenda badala ya kuwalipa fidia kidogo isiyolingana na mali zao wanazoziacha? • Je, ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza ili wananchi waliowekewa alama ya kubomolewa nyumba zao waanze maandalizi kwenye maeneo watakayohamia? • Je, ni lini Serikali itatengeneza upya madaraja ya Ruvu, Mvuha na Dutumi yaliyomo kwenye barabara hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa madaraja hayo ni mabovu sana na yanaweza kusababisha ajali kwa wanaopita hapo?

Supplementary Question 1

MHE. PROSPER J. MBENA: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Pia nifanye marekebisho kidogo Mheshimiwa Waziri alipozungumzia Jimbo langu mimi ni Mbunge wa Morogoro Kusini siyo Morogoro Mjini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa Serikali imekubali kufanya matengenezo ya mara kwa mara katika barabara ya Bigwa mpaka Kisaki ili iweze kupitika wakati wote; na kwa kuwa hivi sasa kuna tatizo kubwa katika sehemu ya Milengwelengwe katika Kata ya Mngazi, usafiri umekuwa mgumu barabara imeharibika. Je, Waziri yuko tayari kuagiza Mkandarasi pamoja na Meneja wa TANROAD Morogoro kwenda haraka eneo hilo na kufanya matengenezo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa nini Serikali isirahisishe matengenezo ya mara kwa mara katika barabara hii kwa kuruhusu kutengeneza vitengo vya matengenezo ya barabara katika Tarafa tatu ndani ya barabara hii ya Bigwa hadi Kisaki ili kurahisisha matengenezo ya barabara? Ahsante sana.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na Mheshimiwa Mbena kwamba Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro anatakiwa aende haraka eneo la Ilengwelengwe kuhakikisha kwamba mawasiliano kati ya Kisaki na Morogoro Mjini yanapitika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili nimepokea ushauri wake, ngoja tupeleke kwa wataalam waangalie, wakachakate waone uwezekano wa kulitekeleza hilo. Nadhani anakumbuka kwamba zamani tulikuwa na vikosi vya PWD au tulikuwa tunajulikana zaidi PWD na baadaye tulivyoondoa na TANROADS ikaunda hiyo ofisi za Mikoa na ofisi za Mikoa zinafanya kazi zile zile ambazo PWD ilikuwa inafanya kazi zamani. Hata hivyo, kama nilivyosema ngoja nilichukue hilo wazo likachakatwe halafu tuone tutasonga mbele vipi.