Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mendard Lutengano Kigola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Ujenzi wa Vituo vya Afya Kata za Mninga na Mtwango bado haujakamilika, hivyo wananchi wa Kata hizo wanaendelea kupata shida ya matibabu:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu?

Supplementary Question 1

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri. Hivi vituo vilianza miaka mingi sana, sasa hivi ni miaka tisa bado havijakamilika na mimi swali langu nimesema ni lini sasa Serikali itamaliza ujenzi huu kwa sababu umechukua muda mrefu sana? Hilo ni swali la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imesema itapeleka Sh.35,500,000 na imeshapeleka Sh.8,000,000 tu, bado Sh.24,000,000 bado. Je, ni lini Serikali sasa itapeleka hii fedha Sh.24,000,000 ili ujenzi ule ukamilike? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge, tulipokuwa kule site; miongoni mwa maeneo tuliyotembelea ni Sekta ya Afya katika Jimbo lake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli hivi sasa imepelekwa shilingi milioni nane, bado takriban shilingi milioni 24. Hata hivyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge; hivi leo asubuhi nilikuwa naongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Bwana Shemdoe. Katika mambo ambayo tumekubaliana ni kwamba atenge fedha kwa kadri inavyowezekana kuhakikisha vituo hivi vinakamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, najua wazi kwamba Jimbo la Mufindi Kusini ni miongoni mwa Halmashauri tajiri ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rasilimali walizonazo zikisimamiwa vizuri tutaweza kufanya vitu vingi zaidi. Kwa hili Mkurugenzi amenipa commitment leo hii asubuhi wakati naingia getini, amesema kwamba atashirikiana na Waheshimiwa Wabunge ahakikishe miradi yote ambayo bado haijakamilika watumie fedha, own source, wakamilishe miradi yote wasiwe na viporo tena vinavyoendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itasimamia vizuri, lakini kwa sababu na wao wamejipanga vizuri, yeye na Mheshimiwa Mgimwa, nadhani hakuna kitu kitakachoharibika katika Halmashauri yao kwa sababu ni miongoni mwa Halmashauri tajiri, own source yao ni kubwa kuliko jambo lingine lolote.

Name

Cosato David Chumi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafinga Mjini

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Ujenzi wa Vituo vya Afya Kata za Mninga na Mtwango bado haujakamilika, hivyo wananchi wa Kata hizo wanaendelea kupata shida ya matibabu:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu?

Supplementary Question 2

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kuniona. Nami naomba kuuliza swali dogo la nyongeza. Hospitali ya Mji wa Mafinga inahudumia Halmashauri mbili za Wilaya ya Mufindi na Mji wa Mafinga. Hata hivyo, katika fedha za Basket Fund, Halmashauri ya Mji wa Mafinga inapokea kiasi kidogo kiasi kwamba inaathiri utendaji wa Hospitali ya Mafinga ambayo inahudumia Halmashauri zote mbili. Je, ni lini Serikali itaongeza fedha za Basket Fund kwa ajili ya Hospitali ya Mji wa Mafinga ambayo inahudumia halmashauri zote mbili? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, anachosema Mheshimiwa Chumi, siyo jambo la uongo. Ni kweli Halmashauri ya Mafinga pale ukiangalia ule Mji, wananchi wa Mufindi wote wanakuja kutibiwa pale Mafinga. Bahati mbaya ukifanya comparison; ulinganifu wa Basket Fund ya Mafinga na Mufindi, Mafinga Basket Fund yao ni ndogo, lakini wagonjwa wote wanakuja kutibiwa Mafinga. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, scenario hiyo iko sambamba na kule Tarime, Halmashauri ya Mji wa Tarime na Halmashauri ya Tarime nanii, kwamba ya Mji ina fedha kidogo, lakini Halmashauri hii ina fedha nyingi lakini ha-top up nanii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, maeneo ambayo Halmashauri haina Hospitali ya Wilaya lakini kuna hospitali mfano ya Taasisi ya Dini, wanatumia kituo kile kama DDH na wanapeleka fedha. Sasa tujiulize, kama watu wa Mufindi hawana hospitali, wanatumia Hospitali ya Mafinga na kama wangekuwa hawana Mafinga, maana yake kungekuwa na hospitali ya private pale ya DDH, wangeitumia kama hivyo na kupeleka fedha. Kwa nini hapa msikae sasa kufanya harmonization ya jambo hilo kulifanya liwe vizuri?
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuseme kwamba jambo hili tumelichukua na nitalikabidhi katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa dada yangu Mheshimiwa Ummy Mwalimu, tutaangalia nini tufanye. Lengo kubwa ni kwamba mwisho wa siku, Halmashauri ya Mafinga na Hospitali ya Mafinga iweze kujiendesha vizuri kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wale. (Makofi)

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Ujenzi wa Vituo vya Afya Kata za Mninga na Mtwango bado haujakamilika, hivyo wananchi wa Kata hizo wanaendelea kupata shida ya matibabu:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu?

Supplementary Question 3

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kama lilivyo swali la msingi, kwenye Jimbo langu la Kyerwa, wananchi wameanzisha vituo ambavyo wameshaanza ujenzi, wamefika kwenye kumalizia boma. Kwa mfano, kama Kata yangu ya Kimuri, kuna wananchi ambao wamejenga boma limefikia kwenye lenta na wameweza kujenga maboma zaidi ya kumi. Maboma haya yamekaa karibu miaka saba. Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha maboma haya? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nataka nikupe taarifa, Mheshimiwa Bilakwate anapoishi kwake pale wakati mwingine ninapofika pale hata mtandao wa simu anapata nchi ya Rwanda. Bahati mbaya hana Hospitali ya Wilaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya suala hili la maboma, kutokana na ombi lake tumeamua kujenga theater sasa na sehemu ya kupasulia wagonjwa pamoja na kupata huduma nyingine katika Kituo chake cha Afya cha Mulongo. Tumefanya hivi ili eneo lake liweze kupata huduma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tumefanya assessment ya maboma yote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jinsi gani tutayamalizia, yale ya Vituo vya Afya na Zahanati, takriban shilingi bilioni 950 zinahitajika. Katika mwaka huu wa bajeti tumeshatenga karibu shilingi bilioni takriban 95. Lengo kubwa ni kuhakikisha tunamalizia hivi viporo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Local Government Capital Development Grant, tumetenga karibu shilingi bilioni 251, karibu one third ya fedha hizo zinakwenda katika suala zima la umaliziaji wa maboma. Kwa hiyo, nawaagiza Wakurugenzi wote wakiwemo na wa Halmashauri yake; inapofika ile fedha, naomba tuweke mgawanyo mzuri wa jinsi gani tutakavyomalizia maboma haya na siyo ya afya peke yake, hata katika Sekta ya Elimu. (Makofi)

Name

Venance Methusalah Mwamoto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Ujenzi wa Vituo vya Afya Kata za Mninga na Mtwango bado haujakamilika, hivyo wananchi wa Kata hizo wanaendelea kupata shida ya matibabu:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu?

Supplementary Question 4

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize swali dogo la nyongeza. Pamoja na Serikali kufanya jitihada kubwa katika kuhimiza ujenzi wa Vituo vya Afya, kumetokea tatizo kubwa sasa hivi ambalo linakabili vituo ambavyo vimekwisha; ni upungufu wa watoa dawa za usingizi. Kwa hiyo, nataka nijue tu, kwa kuwa Vituo vya Afya vingi vitajengwa katika nchi yetu, Serikali
imejipangaje?

Name

Ummy Ally Mwalimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tanga Mjini

Answer

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mheshimiwa Mwamoto kwa swali lake zuri. Ni kweli tunategemea mpaka mwisho wa mwezi Desemba, takriban Vituo vya Afya 100 vitaweza kufanya upasuaji wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni. Kwa hiyo, tayari tumeshaongea na Chuo Kikuu cha KCMC kwa ajili ya kuendelea kutoa kozi mahususi za wataalam wa usingizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika muda huu pia, wale ambao wako tayari katika maeneo ya kazi, tumeandaa mpango wa kuweza kupewa mafunzo ya haraka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe tahadhari, wataalam wangu wanasema tusifanye mafunzo ya haraka, matokeo yake badala ya kuwaokoa akinamama wajawazito tukawaua. Kwa hiyo, tuna-negotiate muda wa mafunzo haya uwe angalau miezi 9 au 12. Wataalam wamekataa muda usiwe chini ya miezi sita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hilo suala tunalifanyia kazi na naamini Mheshimiwa Waziri wa Utumishi yuko hapa, kwa hiyo, pia atatusaidia katika kuajiri wataalam hawa wa usingizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

Name

Joyce John Mukya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Ujenzi wa Vituo vya Afya Kata za Mninga na Mtwango bado haujakamilika, hivyo wananchi wa Kata hizo wanaendelea kupata shida ya matibabu:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu?

Supplementary Question 5

MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri, mapema mwaka huu alifanya ziara katika Mkoa wa Arusha hususan katika Jimbo la Monduli na akatembelea Vituo vya Afya vya Makuyuni na Kigongoni. Vituo hivyo vilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi na kufikia kwenye lenta na aliahidi kuvimalizia mapema mwaka huu au mwaka kesho. Naomba maoni ya Mheshimiwa Waziri, je, ni lini atatoa fedha hizo za kumalizia Vituo hivyo vya Afya vya Jimbo la Monduli? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli siku ile nilifika Arusha, nikafika Monduli na priority yetu ni kwamba tumeitenga pale na commitment tuliyoifanya ni kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Mto wa Mbu ambapo tumezungumza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, nimewapongeza wananchi kwa juhudi kubwa wanayoifanya katika suala zima la ujenzi wa Vituo vya Afya. Kwa hiyo, ni commitment ya Serikali na tuko katika michakato ya aina mbalimbali, tutaweza kukamilisha mambo haya kwa kadri inavyowezekana.

Name

Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Ujenzi wa Vituo vya Afya Kata za Mninga na Mtwango bado haujakamilika, hivyo wananchi wa Kata hizo wanaendelea kupata shida ya matibabu:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu?

Supplementary Question 6

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika Jimbo la Serengeti, Vituo vya Afya vya Iramba na Nata vimetengewa fedha kwenye mwaka huu wa bajeti pamoja na Hospitali ya Wilaya ambayo imetengewa shilingi milioni 700. Leo ni tarehe 21, tarehe 30 mwaka wa fedha huu tulionao unaisha; na Mheshimiwa Waziri alipokuja pale Jimbo la Serengeti, alituhakikishia kwamba fedha zitakuja. Nini tamko lake kuhusu fedha hizi kutokufika mpaka sasa? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nilikuwa na Mheshimiwa Ryoba Jimboni kwake na tulitembelea ile Hospitali ya Wilaya, nami nilikuwa najua kwamba jana ndiyo angeunga mkono Bajeti ya Serikali kwa sababu ndiyo fedha zenyewe hizi zinazopelekwa kwa wananchi. Sasa tunapokuja site pale tunakubaliana fedha ziweze kwenda, tunapokuja huku katika kupitisha mafungu wenzetu mnasusa hamtaki kupitisha, sio jambo zuri. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Ryoba, tumekwenda pale tumeona matatizo ya wananchi. Sawa! Suala la fedha tutakwenda kulitekeleza na kama tulivyoongea kwa kirefu zaidi, pale ukiangalia kupitia Ofisi yetu na Wizara ya Afya katika lile jengo la pale Mugumu tunafanya ile two in one sword, tutafanya lile na wananchi watapata huduma. (Makofi)

Name

Kasuku Samson Bilago

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Ujenzi wa Vituo vya Afya Kata za Mninga na Mtwango bado haujakamilika, hivyo wananchi wa Kata hizo wanaendelea kupata shida ya matibabu:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu?

Supplementary Question 7

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Jimbo la Buyungu, Wilaya ya Kakonko tumepata ufadhili wa kujengewa vituo vya kisasa vya baba, mama na mtoto kutoka Bloomberg, USA. Ni vituo vya kisasa kabisa. Sasa nataka commitment ya Serikali, vituo vile vinawekewa vifaa vya kisasa na vinahitaji wataalam wa kisasa. Je, Serikali iko tayari kuleta wataalam baada ya vituo hivyo kukamilika?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli Kakonko ni eneo ambalo linapata changamoto kubwa sana. Ndiyo maana siku ile nilivyokuwa naongea na watumishi wetu pale Kakonko mpaka kama binadamu unajisikia huzuni kwa cost load waliyokuwa nayo, ni kubwa zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie, kwa sababu Serikali ipo katika mpango wa kuajiri watumishi wengi; na najua katika Mkoa wa Kigoma tumepeleka watumishi wapatao takribani tisa au 12, kati ya hapo tu kwa Mkoa mzima wa Kigoma, lakini mahitaji ni makubwa zaidi. Ngoja mchakato huu sasa wa ajira hizi mpya utakapotoka tutaangalia jinsi gani tusaidie wananchi wa Kakonko pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili siyo kwa Kakonko peke yake na Mkoa wa Kigoma wote kwa ujumla kwa sababu kuna changamoto kubwa ya wakimbizi, kwa hiyo, huduma inakuwa ni tight sana. Kwa hiyo, lazima tutalichukua jambo hilo; Kasulu, Kakonko, Kibondo, Uvinza na sehemu nyingine, kutoa kipaumbele kwa Mkoa wa Kigoma. (Makofi)