Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Mary Michael Nagu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. DKT. MARY MICHAEL NAGU aliuliza:- Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni mia tatu (300,000,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Katesh, hata hivyo mradi huo bado haujaweza kuwanufaisha wananchi kwa sababu ya gharama kubwa za umeme zinazosababisha pampu za maji kufanya kazi kwa muda mfupi tu. Je, Serikali haioni haja ya kupunguza au kuondoa kabisa tariff zilizopo ili gharama ya umeme iwe chini kidogo na kusaidia kusambaza maji kwa ufanisi?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kujibu swali kwa ufupi lakini kama tunavyotegemea, ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri. Sasa naomba niulize maswali mawili madogo kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, maji ya Mji wa Katesh yanaendeshwa kwa umeme wa grid lakini bado gharama ni kubwa. Naomba Mheshimiwa Naibu Waziri anihakikishie kwamba atatuma wataalam kuona kwa nini gharama ile iko juu ili watu wa Katesh waweze kupata maji kwa sababu kwa sasa hivi wanapata mara katika wiki na ni hatari kwa mji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lingine dogo la pili ni kwamba; ninamshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri huyu kwa kuona umuhimu wa vijiji kuwa na umeme ili wanapochimba visima waweze kusukuma maji kwa nguvu ya umeme. Hata hivyo Wilaya yetu ni moja ya Wilaya ambayo imepata vijiji vichache. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri anaweza kunihakikishia kwamba vijiji vyetu vingi sasa vitapata umeme wa REA na kwamba Mkoa wa Manyara ataanzia na Wilaya ya Hanang? Ahsante.

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kuhusiana na kutuma wataalam wakaangalie kama bei ni halisi, Mheshimiwa Mary Nagu kwanza nakupongeza sana kesho wataalam watakwenda kwenye site wataangalia ili wajiridhishe kama ni sahihi, nitawaagiza waende washirikiane na watu wako walioko kule. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na vijiji ambavyo ameseme Mheshimiwa Mary Nagu, kwanza nakupongeza Mheshimiwa Mary Nagu, wakati wakati wa bajeti yetu ulitupatia vijiji vyako 44 ili tuvipelekee umeme. Sasa napenda kuwahakikishia wananchi wa Hanang kwamba vijiji vyako vyote 44 ulivyotupatia ikiwepo kijiji cha Gocho, kijiji cha Kaltaki, kijiji cha Gawindu pamoja na Kateto na vitengoji vyake vyote vitapata umeme Mheshimiwa Nagu.