Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maftaha Abdallah Nachuma

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA aliuliza:- Bandari ya Mtwara ni Bandari yenye kina kirefu Afrika Mashariki na Kati na Serikali kwa makusudi imeamua kuitupa na kujenga Bandari katika maeneo mengine ya nchi tena kwa gharama kubwa sana:- Je, Serikali ipo tayari kukiri makosa na kuiboresha Bandari ya Mtwara ili korosho zote zisafirishwe kupitia Bandari hiyo kwa lengo la kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam?

Supplementary Question 1

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pia nashukuru kwa majibu sahihi ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri kazungumza hapa kwamba Bandari hiyo ya Mtwara ndiyo itakuwa chanzo cha ufunguzi wa kitu tunachoita Mtwara Corridor, maendeleo ya Kusini mwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Naomba kujua kwamba hili gati linajengwa hivi sasa ni gati moja tu. Mkakati wa Serikali ukoje kuhakikisha kwamba wanamaliza ujenzi wa magati matatu yaliyobaki ili yaweze kukamilika magati manne?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, naomba kujua kwa kuwa Bandari ya Dar es Salaam hivi sasa ina msongamano mkubwa sana na Mtwara sasa hivi hii bandari inajengwa. Je, Serikali ipo tayari hivi sasa kuhakikisha kwamba inapunguza cargo on transit kutoka Bandari ya Dar es Salaam waweze kuruhusu Bandari ya Mtwara ili kuweza kuondoa msongamano hivi sasa? Ahsante.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, magati matatu yaliyobakia mpango wake wa kujengwa kwanza tunataka kushirikisha Sekta Binafsi lakini vile vile kwanza tunataka tuhakikishe kwamba gati hili moja na kwa namna mizigo ilivyo kwa sasa tunadhani kwamba linatosha kwa muda mfupi na wa kati. Baada ya hapo ikishafunguliwa ile reli ya kutoka Mtwara mpaka Mbamba Bay kwa vyovyote vile gati hizi nne lazima ziongezeke. Kwa hiyo, nimshukuru kwa swali hilo, nimepata fursa ya kutoa ufafanuzi zaidi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu Bandari ya Mtwara kutumika kama mbadala wa Bandari ya Dar es Salaam; sababu mojawapo ya kupanua hii gati kama tulivyosema hili gati ni la urefu wa mita 350, ni kubwa sana ili liweze kuruhusu meli kubwa sana ziweze kutia nanga Mtwara. Moja kati ya sababu ni hiyo, kwamba meli zingine kubwa ziweze kutua Mtwara badala ya muda wote kufikiria kuingia Dar es Salaam.