Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Silafu Jumbe Maufi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SILAFU J. MAUFI aliuliza:- Serikali imeamua kutoa elimu ya kompyuta kwenye shule za sekondari nchini lakini vifaa vya kufundishia havitoshelezi na hata Walimu ni wachache katika maeneo mengi ikiwemo Mkoa wa Rukwa, ambapo ni shule mbili pekee za Mazwi na Kizwite Sekondari ambazo zimeshaanzishwa:- Je, Serikali ina mpango mkakati upi wa kufanikisha ufundishaji wa somo hilo kwa tija?

Supplementary Question 1

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Pamoja kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri wa TAMISEMI kuhusu swali langu, nina swali la nyongeza.
Pamoja na jitihada na changamoto walizonazo na kuhakikisha kwamba masomo haya yanapatikana katika maeneo yetu ya Rukwa na hasa katika Mikoa yetu ya pembezoni. Kwa kuwa tumechelewa kupata elimu hii na speed ambayo wanakwenda nayo naona kana kwamba haitaweza kuleta mafanikio mazuri kwa mikoa yetu ya pembezoni. Swali langu dogo napenda kuuliza kwa niaba ya Mkoa wa Rukwa, ni lini sasa Wilaya ya Nkasi na Wilaya ya Kalambo masomo hayo yatafikishwa kwani Makao Makuu ya Wilaya hizi umeme umekwishafika?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tukiri kwamba suala la kompyuta sasa hivi na elimu ya TEHAMA ni jambo la msingi sana kama tunataka twende katika maendeleo ya kasi. Tumejielekeza sasa hivi, kama jibu langu la msingi lilivyosema kwamba, tutatumia kila liwezekanalo kuhakikisha tunawezesha vijana katika shule hizi kupata elimu hii ya kompyuta.
Suala la Nkasi na Kalambo ni kweli, katika maeneo mbalimbali ambayo tunataka tuyape nguvu hasa ukiangalia mkoa huu una changamoto kubwa sana, jambo hili hata Mheshimiwa Keissy na Mbunge wa Viti Maalum huwa eanalizungumzia sana, siyo hilo tu na mambo mengine.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, naomba nieleze wazi katika michakato ambayo tutaifanya Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kwa sababu Mkoa wa Rukwa ni Mkoa wenye changamoto kubwa sana, tunaita mikoa ya pembeni, tutajitahidi kwa kadri iwezekanavyo katika program zetu Wilaya hizi tuwape kipaumbele, kwa sababu maeneo mengine ya mijini kama vile Dar es Salaam, Arusha na Mikoa mingine ni rahisi zaidi vijana ku-access mambo ya kompyuta kuliko mikoa ya pembezoni. Kwa hiyo, Ofisi ya Rais, TAMISEMI itaupa kipaumbele Mkoa wa Rukwa na hasa katika Wilaya ya Nkasi na Wilaya ya Kalambo.