Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA alijibu:- Kumekuwa na wimbi kubwa la uhalifu unaofanywa na baadhi ya madereva wa bodaboda na bajaji katika maeneo mengi Jijini Dar es Salaam. (a) Je, Serikali mpaka sasa imechukua hatua gani kudhibiti wimbi hili linalokuwa tishio kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri? (b) Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuhakiki na kutambua mmiliki, dereva na mahali zinapopaki bajaji na bodaboda?

Supplementary Question 1

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa niseme kwamba majibu ya Waziri yanaonesha kana kwamba suala la bodaboda limeanza juzi ama jana.
Suala la bodaboda ni la muda mrefu na kero za watu wenye bodaboda zimekuwa ni kubwa kwa wananchi lakini bado Serikali inasema inajipanga kufanya haya na yale wakati bodaboda ni suala la muda mrefu. Ni dhahiri traffic police wameelemewa na usimamizi wa kudhibiti uvunjifu wa Sheria Barabarani kwa waendesha bodaboda. Kwa mfano; bodaboda zina…

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Kwa mfano; Bodaboda zimekuwa zikipita kwenye traffic lights wakati wowote bila kufuata taa. Je, Serikali haioni ni wakati sasa wa kubadili ama kuboresha mikakati yake ili kuimarisha usalama barabarani hususani jinsi ya kusimamia hawa wenye bodaboda?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, nchini Rwanda wenzetu wana utaratibu mzuri wa kusajili madereva wa bodaboda na kusajili vituo ambavyo wanafanyia kazi. Je, ni lini Serikali itasajili hawa vijana wenye bodaboda na maeneo wanayofanyia kazi ili kuweza kubaini watu wanaofanya uhalifu kwa kutumia bodaboda?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali haya yaliyoulizwa nilishayajibu kwenye jibu la msingi. Ninachosema siyo kwamba Serikali inajipanga, ni Serikali imeshachukua hatua hizi na mambo haya yamefanyika kwa mfano, swali la msingi linauliza Dar es Salaam. Pale Dar es Salaam hatua kubwa sana imeshafanywa ya kusajili waendesha pikipiki na haikuishia hivyo tu wamewapa mpaka jezi za kuwatofautisha na mtu mwingine ambaye hakupangiwa katika vituo hivyo. Lakini siyo hilo tu, ukisema tunajipanga ni kama vile pikipiki ni zile zile ambazo zilishasajiliwa. Kama tulishasajili wakija wapya inabidi pia tuendelee kuwasajili ndiyo maana utaona kwamba zoezi hilo linaendelea kuwa endelevu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hii ya waendesha bodaboda kupita kwenye taa, hilo ni jambo la tabia ambalo tumeendelea kuchukua hatua, lakini elimu imeshatolewa na utaratibu ambao wanatakiwa wafuate ulishatolewa, kwa hiyo, tunaendelea kuchukua hatua kwa wale wanaovunja sheria hizo.