Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Peter Joseph Serukamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kaskazini

Primary Question

MHE. PETER J. SERUKAMBA aliuliza:- Jimbo la Kigoma Kaskazini katika Kata ya Ziwani kuna tatizo kubwa la mawasiliano ya simu hasa katika vijiji vya Kalalangobo, Rubabara, Kigalye, Mtanga, Nyantole na Kazinga. Je, ni lini wananchi watapatiwa mawasiliano hayo?

Supplementary Question 1

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, Mfuko wa Mawasiliano Vijijini haujapewa pesa za kutosha lakini Waziri anasema vijiji hivi vimeingia kwenye Mfuko wa Mawasiliano Vijijini. Je, nataka kujua kama kweli umeingia kazi hii inaaza lini?
Swali la pili, nilidhani Serikali ingekuja na jibu la kusema badala ya kutegemea bajeti ya Serikali, waongee na makampuni ya simu kama Halotel, Airtel, Vodacom na Tigo ili waweze kupeleka mawasiliano kwenye vijiji hivyo kwasababu mbele ya Kazinga kuna Mwamgongo ambayo Mwamgongo tayari kuna mawasiliano na huwezi kufika Mwamgongo lazima uanzie Kazinga. Kwa hiyo, nilitarajia Serikali badala ya kutegemea bajeti peke yake, nikuombe uende ukaongee na makampuni ya simu ili yaweze kupeleka huduma hiyo kwenye vijiji hivyo.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kama nilivyoeleza katika jibu la swali la msingi kwamba ujenzi wa Miundombinu kwa ajili ya mawasiliano utafanyika mara baada ya fedha za mradi zitakapopatikana na vijiji hivi vyote tulivyovitaja tayari vimo katika mpango, vimeingia katika mpango vinasubiri upatikanaji wa fedha. Lini? Ni mara fedha zitakapopatikana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ombi lake la pili, labda tu nimfahamishe kwamba, mfuko wa mawasiliano kwa wote unatekeleza miradi mbalimbali kupitia Kampuni hizo hizo za Halotel, Tigo, Airtel na Vodacom, wao hawatekelezi wenyewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, makampuni haya yanapata ugumu wa kupeleka mawasiliano katika vijiji kwa sababu wanasema havina faida na hivyo Serikali inatoa ruzuku kupitia mfuko huu wa mawasiliano kwa wote na fedha zinapopatikana tunatangaza tender na makampuni hayo ndiyo yanayoomba hizo zabuni kupeleka mawasiliano hayo katika maeneo hayo.
Kwa hiyo, nadhani ni kweli Halotel, Airtel, Voda hata kama tutakwenda kuwashawishi siyo rahisi wao kukubali kwasababu wanajua hakuna faida katika maeneo hayo na hivyo inahitajika ruzuku ya Serikali na ruzuku ya Serikali tunaitoa kupitia mfuko huu wa Mawasiliano kwa Wote.