Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sixtus Raphael Mapunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA aliuliza:- Kwa zaidi ya miaka kumi sasa Serikali imejenga jengo la ghorofa moja kwa ajili ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga lakini jengo hilo bado halijakamilika, ujenzi umesimama kwa muda mrefu hali inayosababisha jengo hilo kuharibika na kuanza kupoteza ubora wake. Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo?

Supplementary Question 1

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Serikali kwa kutenga hiyo milioni 250 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Kutenga fedha ni jambo moja na kulipeleka ni jambo lingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ikumbukwe kwamba mwaka wetu wa bajeti unaanza mwezi Julai, unaisha mwezi Juni, kuchelewa kuipeleka hiyo pesa kwa namna yoyote ile kutaathiri ujenzi wa hilo jengo hasa ikizingatiwa gharama zinaweza zikabadilika.
Je, Serikali inawahakikishia vipi wananchi wa Mbinga kwamba pesa hii itakwenda kwa wakati na ndani ya mwaka wa bajeti wa 2017/2018 jengo likatakamilika? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge mwenyewe na wananchi wa Mbinga, kwa sababu Mbunge unakumbuka ulikuja mpaka ofisini kwangu kwa shida kubwa sana za Jimbo lako na eneo lako. Mwaka huu umepambana mpaka umepata shilingi milioni 250 ambayo kutokana na maombi yako tumeiweka katika bajeti ya mwaka huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni commitment ya Serikali, kwamba tutakapofika mwezi wa Saba mpaka kipindi ambacho tutakachoenda nacho hicho sasa nikuhakikishe kwamba Serikali itajitahidi kwa kadri iwezekanavyo In Shaa Allah, tutajitahidi fedha zitaenda na nikuombe kwamba usimamizi uwe karibu kama ulivyokuwa makini jengo hilo liweze kukamilika kwa ajili ya wananchi wa Mbinga.

Name

Joseph Roman Selasini

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Rombo

Primary Question

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA aliuliza:- Kwa zaidi ya miaka kumi sasa Serikali imejenga jengo la ghorofa moja kwa ajili ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga lakini jengo hilo bado halijakamilika, ujenzi umesimama kwa muda mrefu hali inayosababisha jengo hilo kuharibika na kuanza kupoteza ubora wake. Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mheshimiwa Mwwenyekiti, Serikali inapochelewesha kupeleka fedha ambazo ziko kwenye bajeti kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi mbalimbali za Serikali kama Ofisi za Wakuu wa Wilaya na za Halmashauri inasababisha variation katika ujenzi wa ofisi hizi na kwa sababu hiyo Serikali inaingia katika matumizi makubwa zaidi katika kumalizia.
Je, kwa nini Serikali isitoe kwa mkupuo fedha hizo ofisi hizo zikamalizika zote kwa pamoja ili Halmashauri pamoja Wilaya hizo zikawa na ofisi na Serikali ikaokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa njia ya variation?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, wazo la Mheshimiwa Selasini ni wazo zuri na ndiyo maana nimesema mwaka huu tumetoa karibu shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi huo, lakini unaangalia jinsi gani kila sehemu ina eneo lake la kimkataba la ujenzi. Ndiyo maana hapa tukusema kila Mbunge ataanza kupinga kelele.
Kwa hiyo, ni wazo zuri tutaenda kulifanyia kazi lengo kubwa ni kwamba tumalize haya matatizo yote ya ofisi wananchi na wataalam wetu waweze kupata huduma kwa hiyo ni wazo zuri na Serikali tunaendelea kupeleka fedha kwa kadri tunavyokusanya na mimi naamini kwamba utafika muda ofisi nyingi zitakamilika na Watendaji wetu watakuwa katika mazingira mazuri ya kufanya kazi.

Name

Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Primary Question

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA aliuliza:- Kwa zaidi ya miaka kumi sasa Serikali imejenga jengo la ghorofa moja kwa ajili ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga lakini jengo hilo bado halijakamilika, ujenzi umesimama kwa muda mrefu hali inayosababisha jengo hilo kuharibika na kuanza kupoteza ubora wake. Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo?

Supplementary Question 3

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kaliua haina Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya anatumia Ofisi ya Tarafa ambayo ina hali mbaya na ni chumba kimoja kidogo wanajibana pale. Ofisi ya Wilaya imeanza kujengwa tangu mwaka 2012 na imesimama mwaka 2014 mpaka leo haijaendelezwa. Naomba kujua Serikali ina mpango gani wa kutoa fedha ya kutosha ili Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikamilike na Mkuu wa Wilaya aweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi? Ahsante.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, alichosema Mheshimiwa Sakaya ni kweli na ndiyo maana nimesema kwamba sasa hivi tunajitahidi kupeleka fedha na hata katika Halmashauri yake anafahamu tumeshapeleka milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Halmashauri Kaliua. Hiyo ni commitment ya Serikali kwa Kaliua. Angalia kipindi hiki cha muda mfupi tumepeleka shilingi milioni 700 lakini najua Ofisi ya DC bado haijakamilika. Hii tunalichukua kuangalia jinsi gani tumefanya allocation ya funds niangalie kama Kaliua katika suala la jengo la Mkuu wa Wilaya hali ikoje halafu tutasukuma ili jengo liweze kukamilika. Ofisi hizi zilisimama muda mrefu na sasa hivi nimetoa commitment kubwa ya Serikali kupeleka kwa ajili ya umaziaji wa majengo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo usiwe na mashaka Dadangu tutajitahidi kwa kadri iwezekanavyo.

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA aliuliza:- Kwa zaidi ya miaka kumi sasa Serikali imejenga jengo la ghorofa moja kwa ajili ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga lakini jengo hilo bado halijakamilika, ujenzi umesimama kwa muda mrefu hali inayosababisha jengo hilo kuharibika na kuanza kupoteza ubora wake. Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo?

Supplementary Question 4

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kuuliza swali ndogo tu la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jengo la Mkuu wa Wilaya ya Maswa limeshajengwa lakini limebakia umaliziaji. Mheshimiwa Naibu Waziri alishafika hapo na kuliona sasa anaweza kutuhakikishiaje kwamba mwaka unaoanza wa fedha, fedha kidogo kwa ajili ya umaliziaji zimetengwa ili Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa aweze kuhamia kwenye jengo hilo?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge mwaka huu wa fedha unaokuja tutamaliza lile jengo la Mkuu wa Wilaya, tuna kila sababu kuhakikisha Wakuu wa Wilaya wetu majengo yao yote yanakamilika na tumejipanga katika hilo, Mheshimiwa Ndaki wala usihofu tutajitahidi kwa kadri iwezekanavyo ile kazi kubwa iliyobakia pale tuweze kuiimaliza ili Mkuu wetu wa Wilaya afanye kazi katika mazingira rafiki. (Makofi)