Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amb Dr. Diodorus Buberwa Kamala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA (K.n.y. MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO) aliuliza:- Ibara ya 89 hadi 101 ya Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki inazitaka nchi wanachama wa Afrika Mashariki kubadilishana uzoefu (exchange of information on technological development and research findings). (a) Je, ni taarifa zipi kiutafiti ambazo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeshirikiana? (b) Je, ni taarifa zipi za sekta ya kilimo na mifugo ambazo nchi zimeshirikiana? (c) Je, ni watumishi wangapi waandamizi kutoka Tanzania ambao wamepata ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Supplementary Question 1

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki katika kushirikiana katika masuala ya chakula na mifugo, waliipitisha mpango kazi wa usalama wa chakula, je, utekelezaji wa mpango huo umefikia wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, wakuu wa nchi pia katika kikao chao walitoa mapendekezo ya kuanzisha ufugaji wa kisasa katika nchi za Afrika Mashariki, je, utekelezaji wake umefikia wapi? (Makofi)

Name

Dr. Susan Alphonce Kolimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mpango kazi wa chakula na utekelezaji wa usalama wa chakula katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulijadiliwa na wakuu wa nchi, kwa sasa hivi ni kwamba kwa utaratibu wa sheria na kanuni za Jumuiya ya Afrika Mashariki, nchi husika zinachukua uzoefu na makubaliano waliokuwa wamefikia wakuu wa nchi ili kutekeleza lile waliokubaliana nalo. Nafikiri katika suala hili Wizara ya Kilimo ambayo ndiyo Wizara ya kisekta inaweza kuwa na jibu sahihi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la ufugaji wa kisasa zimechukuliwa jitihada za makusudi za kuhamasisha wakulima na wafugaji hasa wa kuku ili kuweza kujifunza kutoka kwenye nchi hizi za Jumuiya kuweza kupata uzoefu wenzao wanafanyaje ili kuweza kuendeleza area hii ya ufugaji wa kisasa. Wafugaji hawa ni wafanyabiashara wanaweza kuwa wakubwa na wadogo na wameweza kuwa wamejifunza katika mikutano ile ya wafanyabiashara ambayo huwa inaitwa katika East African Council katika jumuiya ili kuweza kupeana uzoefu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kutokana na mikutano hii wanaweza kujadili jinsi wenzao kwenye nchi zinazotoka kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki wanavyofanya basi na wao wanaweza kujifunza. Ninachoweza kusema kwamba Tanzania kama Tanzania wanafanya vizuri katika area hii ya ufugaji wa kisasa na hasa kuku.