Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Angelina Adam Malembeka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza:- (a) Je, ni lini Serikali itajenga viwanda kwa ajili ya malighafi ya karafuu? (b) Je, Serikali haioni kuwa kwa kujenga viwanda hivyo hapa nchini itapunguza kusafirisha karafuu nje ya nchi kinyume na utaratibu?

Supplementary Question 1

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, yenye data na yamenifurahisha. Pamoja na majibu hayo mazuri nina swali moja la nyongeza na ombi moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ahadi ya Mheshimiwa Rais juu ya kujenga viwanda ili kutoa ajira, kujenga uchumi na kutumia malighafi za eneo husika lilizungumzwa bila ubaguzi wowote na kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri katika majibu yake amesema jukumu la Serikali ni kuhamasisha na kuweka mazingira mazuri ya uwezeshaji na ujenzi ni jukumu la sekta binafsi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi nimekuwa nikisikia Wizara hiyo ikisema hapa na kupiga debe kuhusu ngozi, pamba, matunda, sukari, ndizi, mihogo hadi pilipili sijasikia hata siku moja Wizara hiyo ikizungumza kuhusu mchakato wa karafuu. Ni lini sasa Mheshimiwa Waziri ataanza kuweka hamasa ya kasi ili Zanzibar tupate kiwanda cha kuchakata karafuu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu sasa, kwa kuwa suala la viwanda ni la nchi nzima bila kujali suala la Muungano na kuna vitu ambavyo vimefanyika Zanzibar bila kujali suala la Muungano nikitolea mfano wa barabara iliyojengwa round about ya Amani hadi Mtoni ambayo ilijengwa kwa fedha ya Muungano na kupewa jina la Mkapa Road, kwa nafasi hii kwa niaba ya wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Unguja naomba tujengewe kiwanda cha karafuu Zanzibar ili vijana wetu wapate ajira. Ahsante. (Makofi)

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Answer

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge lile la kwanza ambalo litajibu na namba mbili, kuhamasisha uchumi wa viwanda nchi nzima ni jukumu la Wizara yangu na nitashirikiana na Mheshimiwa Mbunge twende Zanzibar niweze kuhamasisha kwa nguvu ileile ambapo nimeanzia sehemu nyingine. Katika utaratibu huo nitawahasisha wawekezaji ambao najua wapo kusudi tu- take advantage ya karafuu, mwani na michaichai kusudi tu- take advantage ya viungo hivi na manukato. (Makofi)