Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Khadija Nassir Ali

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KHADIJA NASSIR ALI aliuliza:- Kila mwaka Tanzania inaagiza tani laki nne za mafuta ya kula wakati tuna malighafi za kutosha kama vile alizeti, ufuta na kadhalika kwa ajili ya kuzalisha mafuta hayo. Je, Serikali haioni haja ya kuchukua hatua za makusudi za kutumia malighafi hizo ipasavyo na kuokoa fedha za kigeni zinazopotea nchini?

Supplementary Question 1

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kila Wilaya nchi nzima vijana wametenga maeneo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi. Je, Serikali lini itaona umuhimu wa kutumia maeneo haya kwa ajili ya uzalishaji wa malighafi hizo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, tumekuwa tukiona Serikali ikihamasisha wakulima wetu kulima mazao mbalimbali ya kibiashara bila ya kuwa na mikakati mizuri ya masoko na matumizi. Je, ni nini kauli ya Serikali juu ya hili? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kweli Serikali imesisitiza na imeendelea kutenga maeneo kwa ajili ya vijana pamoja na wajasiriamali wengine. Serikali katika kusaidia hilo, kwa mfano katika bajeti ya mwaka 2017/2018 tayari kupitia SIDO imetenga shilingi bilioni saba kwa ajili ya kujenga sheds yaani sehemu za kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuweka viwanda. Maeneo hayo yapo katika Mikoa ya Kagera, Geita, Simiyu, Mtwara, Manyara na Katavi, hiyo ni kwa kuanzia. Kwa hiyo, niseme tu kwamba itakapotokea sheds hizo zimekamilika, tutawahamasisha vijana pia kutumia fursa hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa masoko, tumekuwa tukiendelea kuhakikisha kwamba tunalinda wazalishaji wa mafuta walioko nchini lakini vilevile kwa kushirikiana na nchi zinazotuzunguka kuona kwamba mazingira ya biashara ya mafuta ya kula ushindani wake ni ule ambao hauiathiri nchi yetu. Kwa misingi hiyo, kwa kuangalia mafuta ya kula ambayo yanaagizwa kutoka nje na uhalisia wa kodi ambazo zinatolewa tayari kuna timu inafanya utafiti ili kuhakikisha kwamba masoko yanakuwa ya uhakika na watu wanazalisha kwa faida.