Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ajali Rashid Akibar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. AJALI R. AKBAR aliuliza:- Wilaya ya Newala ni Wilaya kongwe ambayo hata utawala wa Wajerumani ulizingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi ambao Wilaya hiyo imepangwa tangu enzi lakini hivi karibuni TANROADS wamefanya upanuzi wa barabara ulioelekea hadi Chitandi – Masasi. Je, kwa nini Serikali kupitia TANROADS Mtwara isifanye tathmini ya nyumba za wakazi hao na kuwalipa fidia? MHE. AJALI R. AKBAR aliuliza:- Wilaya ya Newala ni Wilaya kongwe ambayo hata utawala wa Wajerumani ulizingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi ambao Wilaya hiyo imepangwa tangu enzi lakini hivi karibuni TANROADS wamefanya upanuzi wa barabara ulioelekea hadi Chitandi – Masasi. Je, kwa nini Serikali kupitia TANROADS Mtwara isifanye tathmini ya nyumba za wakazi hao na kuwalipa fidia?

Supplementary Question 1

MHE. AJALI R. AKBAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sina tatizo kuhusu barabara hii kupitia kwenye milima, tatizo langu ni uwepo wa sheria kwamba kama nilivyozungumza kwenye swali langu la msingi, mji huu wa Newala upo tangu mwaka 1800; kama wakati ule ilikuwa inaitwa Dutch East Africa. Hii sheria ya mwaka 2007 imekuta wananchi wale wakiwa na taasisi zile katika uwepo halali. Kuna polisi, mabenki na wananchi, maana yake walikuwepo kisheria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake wanachopinga wao ni kwamba hii sheria imewakuta wao wakiwepo kisheria. Kwa hiyo, swali langu la msingi, je, ni lini TANROADS watafanya mazungumzo na wananchi hawa wa Newala ili tukaondoe kesi ile Mahakamani?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kutokana na ufinyu wa Mji wa Newala, je, sasa TANROADS wako tayari badala ya kupitisha ile barabara Newala Mjini, wapitishe Kiduni hadi Nambunga kwa Mheshimiwa Mkuchika ili kuepuka mrundikano wa barabara katika ya mji?

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge, anafuatilia sana maendeleo ya Newala na anajua eneo hili ambalo analizungumza pia ni maarufu sana kwa uzalishaji wa korosho.
Kwa hiyo, namuahidi kwamba sisi Serikali tuko tayari kwenda kufanya mazungumzo na ninampongeza sana kwa nia yake thabiti ya kuhakikisha kwamba kama shauri hii tunalimaliza, itaharakisha pia ujenzi wa barabara. Kwa hiyo, tuko tayari kuzungumza ili tulimalize ili wananchi hawa waweze kupata haki zao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa ule utaratibu ambao wanafikiria, na mimi eneo lile nilitembelea, ni kwamba tukiweza kupitisha bypass kwenye eneo hilo, tutaweza pia kuufanya mji upendeze lakini pia kupanua huduma, kwa hiyo, tutakuwa tuko tayari kuhakikisha kwamba tunarekebisha michoro na saa nyingine wananchi waweze kupata haki zao. Ahsante. (Makofi)