Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:- Upembuzi yakinifu wa kutumia chanzo cha maji cha Mto Ibofwe ili kumaliza tatizo la maji katika Kata za Magulilwa, Luhota, Mseke, Ifunda, Mgama na Maboga ulifanyika kati ya mwaka 1995 – 2000 chini ya usimamizi wa Mbunge wakati huo, Mheshimiwa George Mlawa na bajeti ya utekelezaji wake kupitishwa na Bunge hili ili uwe katika kipindi cha mwaka 2000-2005/2005-2010. Je, ni tatizo gani lililofanya mradi huo usikamilike na kuwaacha wananchi wakiendelea kuteseka wakati Bunge lilikwishapitisha bajeti ya mradi?

Supplementary Question 1

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nitoe masikitiko makubwa sana kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri, ambapo tarehe 8 Juni, 2016 niliuliza swali kuhusu vijiji na kata hizo hizo na aliyekuwa Naibu Waziri na sasa ni Waziri mwenye dhamana TAMISEMI alinipa majibu ambayo yalikuwa yanaeleza kwamba vijiji hivyo vimetengewa bajeti ya shilingi milioni 49.5 ambayo itatekelezwa mwaka 2016/2017. Mpaka sasa hivi hakuna kinachoendelea, ni Bunge hili hili ambalo linatoa majibu hayo na leo tena nimepewa asilimia hiyohiyo 49.5 kwamba itatekelezwa 2018/2019. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu, ni lini Serikali itapeleka pesa kwa wananchi hawa, toka mwaka 1995 mpaka leo ni upembuzi yakinifu unafanyika, ni lini hawa wananchi watapata maji? (Makofi)
MheshimiwaMwenyekiti, swali la pili, ni kwa nini hawakufanya upembuzi wa kina wakati bajeti ilitengwa? Ahsante. (Makofi)

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, ni kweli kwamba usanifu wa kina haukufanyika ule wa zamani, lakini kwa sasa tunatarajia usanifu kina utafanyika mwaka 2018/2019 kwa ajili ya utekelezaji wa kumaliza kabisa matatizo ya maji kwenye maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ambalo lilikuwa ndiyo la kwanza, ni kwamba kazi ambazo zimefanyika kuanzia 2016 mpaka Desemba, 2017 nimesema hapa kwamba tumejenga visima sita katika Kata za Magulilwa, Luhota, Maboga na Mgama. Hii kazi imefanyika na taarifa hizi zimetoka kule kule kwenye Halmashauri yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, taarifa za kina zaidi namuomba sana tushirikiane naye baada ya kikao hiki ili tuweze kushauriana vizuri namna bora ya kuhakikisha kwamba tunamaliza matatizo ya wananchi kwenye maeneo hayo.

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:- Upembuzi yakinifu wa kutumia chanzo cha maji cha Mto Ibofwe ili kumaliza tatizo la maji katika Kata za Magulilwa, Luhota, Mseke, Ifunda, Mgama na Maboga ulifanyika kati ya mwaka 1995 – 2000 chini ya usimamizi wa Mbunge wakati huo, Mheshimiwa George Mlawa na bajeti ya utekelezaji wake kupitishwa na Bunge hili ili uwe katika kipindi cha mwaka 2000-2005/2005-2010. Je, ni tatizo gani lililofanya mradi huo usikamilike na kuwaacha wananchi wakiendelea kuteseka wakati Bunge lilikwishapitisha bajeti ya mradi?

Supplementary Question 2

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Arusha una majimbo ambayo kijiografia yana mazingira magumu sana, hasa Jimbo la Ngorongoro na mara nyingi Mawaziri mmekuwa mkifika pale mmeona mazingira yale na kumekuwa na tatizo kubwa sana la upatikanaji wa maji kwenye vijiji vilivyoko katika Jimbo la Ngorongoro.
Je, Serikali sasa ina mkakati gani wa haraka wa kuhakikisha Jimbo la Ngorongoro linatizamwa kwa upekee na wananchi wake wanaweza kupata maji?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali ambalo limeelekezwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuhusiana na utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya Ngorongoro kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Januari, tumesaini mkataba wa milioni 270 kwa ajili ya mradi wa maji katika Halmashauri ya Mji wa Ngorongoro, sasa hivi tunafanya design ambapo tunatarajia mwezi Aprili, tutasaini mkataba mkubwa ambapo tutapeleka maji zaidi ya vijiji tisa likiwemo eneo la Mageli. Kwa hiyo, suala la maji upande wa Ngorongoro linashughulikiwa na tutahakikisha kwamba asilimia 85 itakapofika 2020 inafikiwa pia katika Halmashauri ya Ngorongoro. (Makofi)