Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Tatizo la uhaba wa watumishi wa Idara ya Afya Urambo linaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. (a) Je, Serikali inachukua hatua gani za dharura katika kuliondoa tatizo la uhaba wa watumishi wa Idara ya Afya Wilayani Urambo? (b) Je, Serikali inaweza kuchukua vijana wa Urambo na kuwapeleka vyuoni kusoma kwa makubaliano ya kurudi kufanya kazi Urambo?

Supplementary Question 1

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyingeza, lakini kabla ya hapo naomba uniruhusu kwa kifupi sana nimshukuru Naibu Waziri Mheshimiwa Kandege alifika Urambo na kujionea mwenyewe, ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri, karibu tena, ulifanya kazi nzuri na kusababisha tupate wafanyakazi 17 kama ulivyosema lakini sasa swali la nyongeza ni kama ifuatavyo:-
Kwa kuwa Serikali imeona uhaba wa wafanyakazi uliopo na kutokana na wagonjwa wengi kutoka jirani zangu Kaliua ambako hawa Hospitali ya Wilaya wakiwemo kutoka Ulyankulu, Uyui, Uvinza. Naomba kuwauliza Serikali kama wako tayari kuongeza wafanyakazi ili tuendelee kutoa huduma nzuri?
Swali la pili ni kwamba, kutokana na ongezeko la wagonjwa wengi kutoka Kaliua, Uyui, Uvinza ikiwemo Ulyankulu, je, Serikali iko tayari kutuongezea fedha ikiwemo fedha za Busket Fund ili tuweze kumudu ongezeko la wagonjwa ambao wanatoka jirani? Ahsante sana.

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba wa dhati nipokee pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta.
Mheshimiwa Naibu Spika, kimsingi tulifanya ziara kule na tukajionea kazi nzuri ambayo naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana jinsi ambavyo anahangaika na suala zima la afya za wananchi wa Urambo na tulipata fursa ya kutembelea Hospitali ya Wilaya na katika moja ya ombi ambalo Mheshimiwa Mbunge aliwasilishwa kwetu Ofisi ya Rais, TAMISEMI ni pamoja na suala zima la kubadilishiwa matumizi kiasi cha shilingi milioni 150 ili ziweze kutumika katika kujenga wodi ambayo ni Grade A wazo ambalo tumelichukua na punde tutalifanyia kazi ataweza kupata majibu ili pesa ile iweze kutumika.
Kuhusiana na suala zima la uhitaji wa watumishi ili kukidhi haja ya wagonjwa ambao wanasafiri kutoka Wilaya nyingine kwenda Wilaya ya Urambo kwanza naendelea kumpongeza, ukiona wagonjwa wanakuja kwako maana yake huduma ambayo inatolewa na hospitali yako ni nzuri ukilinganisha na wengine.
Kwa nia hiyo hiyo njema na katika kuhakikisha kwamba tunakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Urambo, wewe ni shuhuda tulikubaliana, jitihada zinafanywa na Serikali hivi karibuni pesa zitakuja kwa ajili ya kulimalizia ile wodi ambayo ilikuwa imeanzishwa kutoka Wizara ya Afya.
Lakini kama hilo halitoshi, naomba niungane mkono kabisa na Mheshimiwa Magret Simwanza Sitta kwamba iko haja ya kutazama kwa kadri nafasi itakavyoruhusu watumishi wakipatikana ili kuweza kuongeza maana ukienda Kituo cha Afya Usoke pale tumeona kazi nzuri ambayo inafanyika na itakamilika hivi karibuni iko haja ya kuongeza watumishi pale watakapokuwa wamepatikana.