Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bupe Nelson Mwakang'ata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza:- Serikali ilipanga kujenga na kupanua Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga Mjini:- Je, ni lini ujenzi huo utakamilika pamoja na kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka uwanja huo?

Supplementary Question 1

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa wananchi hawa walifanyiwa tathmini ya muda mrefu mpaka sasa hawajalipwa, nataka kujua, je, ni lini Serikali sasa itawalipa wananchi hawa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa wananchi hawa walifanyiwa tathmini muda mrefu ya nyumba zao na wameshindwa kuziendeleza na kufanya maendeleo. Je, Serikali iko tayari kuwaongezea tathmini ya fidia ili walipwe kiasi kikubwa? (Makofi)

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia maendeleo mbalimbali kwa wananchi wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Waziri alitembelea eneo hili walizungumza na alipata pia taarifa kwamba muda siyo mrefu, wakati wowote wananchi watalipwa hizi fidia. Kwa hiyo, nimwombe tu Mheshimiwa Mbunge avute subira wakati wa hatua za kukamilisha ili tuweze kuwalipa wananchi wale na ujenzi uweze kuanza basi avute tu subira na wananchi wa Sumbawanga nawashukuru kwa uvumilivu.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kulipa kwa ziada inategemea na sheria yenyewe na utaratibu wenyewe. Kwa hiyo, nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge labda kama kuna suala la ulazima basi tuzungumze tuone kwamba je, wanastahili kulipwa ziada kutokana na kuchelewa au iko katika hali gani.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)