Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Wilfred Muganyizi Lwakatare

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Bukoba Mjini

Primary Question

MHE. WILFRED M. LWAKATARE aliuliza:- Serikali imeamua kuhamisha tozo la kodi ya umiliki wa nyumba kutoka Serikali za Mitaa kwenda TRA na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa mapato na bajeti za Halmashauri nyingi nchini zilizokwishapendekezwa na kupitishwa na vikao vya Halmashauri:- • Je, Serikali inazipa Halmashauri ushauri gani wa kitaalam wa hatua za kuchukua ili kuziba pengo hilo la kibajeti? • Kwa kuzingatia uwezo mdogo uliooneshwa na TRA katika kukusanya kodi mbalimbali ambazo wamekuwa wakikusanya kwa mujibu wa sheria. Je, Serikali haioni kwamba uamuzi huu ni kuzidi kuipa TRA mzigo mkubwa ambao hawatauweza?

Supplementary Question 1

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Serikali iliyoyatoa hapa, nina maswali mawili ya nyongeza kama ifutavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na takwimu kubwa alizozitoa ambazo zinaonyesha kupanda kwa mapato ni ukweli usiopingika kwamba yapo maeneo mengi kwelikweli ambayo hayajafikiwa na TRA kwa sababu ya mtandao wake mdogo, kiasi kwamba TRA hata kufanikisha hiki kilichofanikisha imelazimika kuwatumia Maafisa Watendaji wa Kata ambao ni waajiriwa wa Halmashauri hizi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini Serikali isichukue wazo langu la kujaribu kuweka category mbili kwamba baadhi ya tozo hii ya property tax na hasa za majumba makubwa zitozwe na TRA lakini kwa majengo ya chini yatozwe na Halmashauri zetu na hiyo itaongeza ufanisi badala ya kuzi-tight kwenye Majiji 30? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; suala la mapato na makusanyo kupanda limekuwa ni wimbo wa kila siku, kutoka kwenye taarifa za Serikali pamoja na TRA, lakini Bunge kupitia Kamati zake na kupitia kwenye Halmashauri zetu…
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini taarifa zinaonesha Taasisi nyingi za Serikali na Serikali yenyewe na Mashirika pamoja na Halmashauri zetu hata Bunge lenyewe limeshindwa kwenda sambamba na bajeti kiasi kwamba maeneo mengine ina-read zero, zero wakati wanasema wanakusanya sana? (Makofi)

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpomngeze kwa kukiri kwamba anaelewa sasa mapato ya Serikali yamepanda katika nyanja zote kwa kodi zote zinazokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiwemo kodi ya majengo, nakupongeza sana shemeji yangu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hili alilolisema sasa tugawanye kwamba majengo makubwa yakusanywe na Mamlaka ya Mapato na madogo yakusanywe na Serikali za Mitaa, tutajikuta tunatumia nguvu za aina mbili katika eneo moja bila sababu yoyote ya msingi. Serikali yetu na Bunge lako Tukufu tulipitisha Sheria ya Fedha, kwamba kodi ya majengo ikusanywe na Mamlaka ya Mapato kwa lengo la kuimarisha ufanisi wake katika ukusanyaji na ufanisi wake katika matumizi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama Serikali tutaendelea kusimamia sheria hii kuhakikisha kwamba lengo la kuchukua kodi hii linafikiwa na wananchi wetu wanapata huduma stahiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kwamba sasa bajeti hai-reflect mapato. Ni siku mbili zilizopita Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani kwa mwaka huu wa fedha kwa robo tu ya kwanza Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepata zaidi ya shilingi trilioni moja katika bajeti zao. Serikali inafanya vizuri kwenye ukusanyaji lakini pia tunafanya vizuri kupeleka fedha hizi katika kila taasisi ya Serikali yetu. Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. WILFRED M. LWAKATARE aliuliza:- Serikali imeamua kuhamisha tozo la kodi ya umiliki wa nyumba kutoka Serikali za Mitaa kwenda TRA na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa mapato na bajeti za Halmashauri nyingi nchini zilizokwishapendekezwa na kupitishwa na vikao vya Halmashauri:- • Je, Serikali inazipa Halmashauri ushauri gani wa kitaalam wa hatua za kuchukua ili kuziba pengo hilo la kibajeti? • Kwa kuzingatia uwezo mdogo uliooneshwa na TRA katika kukusanya kodi mbalimbali ambazo wamekuwa wakikusanya kwa mujibu wa sheria. Je, Serikali haioni kwamba uamuzi huu ni kuzidi kuipa TRA mzigo mkubwa ambao hawatauweza?

Supplementary Question 2

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kunipa nafasi nimuulize mtani wangu swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha amesema kwamba Serikali inapeleka fedha katika Halmashauri zetu na fedha wanazopeleka kwa upande wa OC ni fedha za mitihani tu. Mfano, Halmashauri yangu ya Mji wa Babati wamepeleka 265,605,000 za mitihani tu, hakuna fedha za OC. Je, nini kauli za Serikali kuendelea kudumaza Halmashauri zetu, Wakurugenzi wanashindwa kuendesha ofisi na ni lini wanapeleka pesa? (Makofi)

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze pia kwa kumpongeza kwa kukiri kuwa tunapeleka fedha kwenye Halmashauri. Kwa sababu swali hili linahitaji takwimu nitamletea takwimu sahihi katika Halmashauri yake tumepeleka kiasi gani kama OC katika utekelezaji wa bajeti. (Makofi)