Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Pascal Yohana Haonga

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbozi

Primary Question

MHE. PASCAL Y. HAONGA aliuliza:- Kigezo kimojawapo cha kuwanyima mkopo waombaji wa mkopo ya elimu ya juu ni kama muombaji alisoma shule za binafsi. (a) Je, Serikali haioni kuwa baadhi ya wanafunzi hulipiwa ada ya shule za binafsi na ndugu, jamaa, marafiki na NGO’s hivyo wanafunzi hao wanapofikia elimu ya juu hushindwa kumudu gharama za elimu hiyo? (b) Je, Serikali ipo tayari kufuta kigezo hicho ili kuwapatia waombaji wa mikopo haki yao ya kupata elimu ya juu?

Supplementary Question 1

MHE. PASCHAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, siku za hivi karibuni tumeisikia Bodi ya Mikopo imeongeza masharti au vigezo vipya kwa wakopaji, kwa mfano wale viongozi wanaojaza fomu za maadili ya viongozi wa umma wakiwepo Madiwani nao pia ni miongoni mwa watu ambao watoto wao wananyimwa mikopo. Kwa kuwa tunajua kabisa kwamba Madiwani hawana mishahara na wanategemea posho ambayo ni kidogo sana je, Serikali haioni kwamba, huu ni unyanyasaji ambao kwa namna yoyote hauvumiliki na hitakiwi kuufumbia macho unaofanywa na Bodi ya Mikopo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, siku za hivi karibuni wote tunajua kabisa kwamba Bodi ya Mikopo imeongeza makato kwa wanufaika wa mikopo. Kwa mfano awali ilionekana kwamba, wanufaika wa mkopo walikuwa wanalipa wanarejesha asilimia nane ya mkopo waliokuwa wamekopa kwa maana ya makato ya asilimia nane, lakini kwa sasa wanakatwa asilimia 15. Hali hii imesababisha wale wanufaika wa mkopo kama walimu na watumishi mbalimbali ambao walikuwa wamebakisha fedha kidogo ambazo walikuwa wanapata mwisho wa mwezi, leo hawana mshahara hata kidogo na kuna watumishi wanaacha kazi. Je, Serikali haioni ni wakati muafaka sasa kurudi kwenye asilimia nane ya makato, ili angalao watumishi hawa waliocha kazi waweze kurudi makazini na maisha yaweze kwenda vizuri? Ahsante sana.

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli alivyosema kwamba katika mwaka huu wa masomo kuna vigezo vimeongezwa kwa ajili ya watu ambao hawastahili kupata mikopo, ikiwa ni pamoja na viongozi wa umma wanaojaza fomu za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma. Lengo la kufanya hivyo ni kwamba, tunajaribu kuhakikisha kwamba mkopo ule unatumika kwa wale ambao hawana uwezo kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuhusu Madiwani kama wana uwezo au hawana uwezo tunajaribu kuangalia kipato chao wanachoweza kupata kwa mwaka na kulinganisha na Watanzania wengine wengi ambao hawana kipato kabisa. Kwa hiyo, lengo ifahamike tu ni kwamba ni kujaribu kutoa fursa kwa wale ambao hali yao ni mbaya zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hitaji la sasa la kwamba waombaji wa mikopo ambao wanatakiwa kurudisha wanakatwa asilimia 10 inatoka kwenye mshahara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilifahamishe Bunge lako Tukufu kwamba mkopo ule ukishachukua kigezo cha pekee cha kwamba unatakiwa kurudisha fedha ni kwamba wewe umekopa, maana yake ilitakiwa pale unapomaliza shule uanze kurudisha.
Sasa kwa muda mrefu sana ule mkopo umekuwa unashindwa kuwanufaisha watu wengi kwa sababu watu wengi hawarudishi na ndio maana sasa tumelazimisha kwamba, ni lazima kwamba, mtu ambaye atakuwa amepata ajira aweze kulipa kwa asilimia 15 ya mshahara wake, lakini vilevile kuna kigezo kingine ambacho tumeweka kwamba, tunatoa kipindi cha mpito au grace period ya miezi 24 toka mwanafunzi amalize shule, lakini baada ya hapo kama hajaanza kulipa tunaanza vilevile kutoza riba ya asilimia
10. Lengo ni kwamba tunahitaji kuufanya mfuko ule uwe endelevu ili wananchi wengi waweze.
Waheshimiwa Wabunge nafahamu kuna baadhi ambao nao wanadaiwa mikopo, katika siku hizi za karibuni tunakuja na orodha ya wale ambao ni wadaiwa sugu. Kwa hiyo, nawaombeni ushirikiano…