Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Suleiman Ahmed Saddiq

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ (K.n.y. MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA) aliuliza:- Amani na utulivu ni muhimu sana katika maisha ya binadamu. Je, ni lini mgogoro wa wakulima na wafugaji katika Wilaya za Mvomero na Kilosa, Mkoani Morogoro utaisha lini ili wananchi waweze kuishi kwa amani na utulivu?

Supplementary Question 1

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Ni kweli kuna juhudi mbalimbali zinazoendelea kufanyika katika Wilaya ya Mvomero kuondoa tatizo la wakulima na wafugaji, na kwa kweli Serikali imefanya kazi kubwa kupitia Waziri Lukuvi, Mheshimiwa Simbachawene pamoja na Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, tunawashukuru Mawaziri hawa, wamefanya ziara mbalimbali. (Makofi)
Swali la kwanza, kwa kuwa juhudi ambazo tunaendelea kuzifanya kama Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero zinahitaji bajeti, na kwa kuwa tayari Mawaziri hawa tumeshawapa bajeti zetu ili tuondoe mgogoro huu na wakulima na wafugaji wawe na maeneo yao. Je, ni lini Serikali itatoa fedha ambazo tuliziomba na fedha zile ziko kwenye bajeti?
Swali la pili, kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kuna mashamba sita yamerudishwa, na mashamba mengine zaidi ya 29 bado hayajarudishwa.
Je, lini Waziri mhusika pamoja na Mheshimiwa Rais, watayafuta yale mashamba yaliyobaki ili tuwagawie wananchi maeneo ya wakulima na wafugaji?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la bajeti, Wizara ya Ardhi pamoja na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwenye bajeti yake imetenga fedha pamoja na mambo mengine kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi, vilevile kwa ajili ya kuweka miundombinu ya huduma za mifugo, kwa ajili ya Wilaya ya Mvomero.
Kuhusu swali la pili, tayari mashamba mengine yameshapelekwa Wizara ya Ardhi ili yaweze kufutiwa hati. Wilayani Kilosa mashamba 73 yenye ukubwa wa ekari 429,625.3 tayari yameshabainishwa na kupelekwa ili yaweze kufutwa. Vilevile Wilayani Mvomero mashamba 84 yenye ukubwa wa ekari 119,382.6 nayo yameshapelekwa Wizara ya Ardhi ili kufanyiwa kazi. Lengo ni kwamba haya mashamba yote yakiweza kufutiwa hati baada ya hapo utaratibu utakaofuata ni kuwagawia Wafugaji na Wakulima ili kuweza kuondoa tatizo kubwa lililopo la ardhi na hatimaye kupunguza migogoro hiyo ya ardhi.