Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Primary Question

MHE. ABDALLAH H. ULEGA aliuliza:- Je Serikali imejipangaje kuwafidia au kuwapa kifuta machozi wananchi wa Kata za Magawa na Msonga katika vijiji vya Makumbaya, Magewa na Msonga ambao mikorosho kwenye mashamba yapatayo ekari 1000 imeangamia kutokana na ugonjwa wa ajabu na kuwaacha wananchi hawana kitu na hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya maeneo wananchi wanaopatwa na majanga kama haya wamekuwa wakilipwa fidia au hata kifuta machozi?

Supplementary Question 1

MHE. ABDALLAH HAMISI ULEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu haya mazuri ya Serikali naomba sasa niulize majibu ya maswali mawili ya nyongeza.
(a) Je, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kuongozana na mimi kwenda Jimboni Mkuranga katika vijiji hivi vya Magawa, Msonga Makumbeya na vinginevyo pata athari hii ili aweze kujionea yeye mwenyewe na kuona namna iliyobora zaidi ya kutusaidia?
(b) Ningeomba niulize Serikali sasa ipo tayari kuhakikisha kwamba viuatilifu kwa maana ya sulfur, iweze kupatikana kwa wingi na kwa wakati katika Jimbo letu la Mkuranga ili kuepusha madhara haya ya ugonjwa wa mikorosho na kuhakikisha uzalishaji mkubwa zaidi ili kuwaondolea wananchi wangu umaskini?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ombi lake la kutaka tuongozane naye kwenda Jimboni tumelipokea na ninamuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa namna ambavyo amekuwa akifuatilia hili suala tayari tulishapanga kufika Mkuranga na kipindi cha bajeti kitakapoisha mimi binafsi nitaongozana naye kwenda Mkuranga ili kujionea hali halisi na kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili ni kweli kwamba kumekuwepo na changamoto ya upatikanaji wa viwatilifu kwa wakati hasa sulfur na huko nyuma tayari kumeshatokea matatizo kwa sababu hiyo, kama nakumbuka mwaka 2011 kulikuwa na changamoto wakatia wa matumizi ya kiatilifu cha aina eugenol 880, lakini kwa sasa Wizara kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho imejipanga vizuri kuhakikisha kwamba viwatilivu hivyo na hasa sulfur zinapatikana kwa wingi na kwa wakati. Hivyo, ninamuahidi kwamba changamoto hii imeshafanyiwa kazi.