Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Halima Abdallah Bulembo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HALIMA A. BULEMBO (K.n.y MHE. KABWE Z. R. ZITTO) aliuliza:- Nchi ya DRC inaitegemea Kigoma kiuchumi kwa kiwango kikubwa hususan katika soko la bidhaa na huduma ya bandari ya Kigoma na hivyo wananchi wengi wa Kigoma kutembelea Congo na wale wa Congo kutembelea Kigoma. Changamoto kubwa ni gharama za biashara kutokana na viza kati ya nchi hizo mbili licha ya kwamba nchi hizo zote ni wanachama wa SADC na nchi za SADC hazina viza kwa raia wake. Je, ni kwa nini Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haziondoi viza kwa raia wake ili kudumisha biashara kati ya wananchi wake kwa lengo la kukuza Kigoma kuwa Kituo cha Biashara cha Maziwa Makuu?

Supplementary Question 1

MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Spika, kwenye majibu ya msingi ya Mheshimiwa Waziri, migogoro ni moja ya sababu inayokwamisha jambo hilo, lakini migogoro hiyo haijazuia wananchi wetu kufanya biashara. Ni kwa nini Serikali isirahisishe movement ya wananchi wetu hasa hasa vijana wa Kitanzania kuchangamkoa fursa ya soko kubwa la Congo ikizingatiwa Congo ni land locked country? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, hivi tunavyozungumza tuna utaratibu mzuri tu ambao unatumika na uko kwa mujibu wa sheria, wa wananchi ambao wanahitaji kufanya biashara, kwa Watanzania ambao wanahitaji kwenda Congo na wale wa Congo ambao wanahitaji kuja Tanzania. Utaratibu uliopo sasa hivi ni utaratibu wa kutumia viza ambazo zinaitwa business visa kwa nchi ya DRC. Lakini hoja ya msingi hapa ilikuwa ni jinsi ambavyo tunaweza kufanya ili kuwa na utaratibu ambao utakuwa ni mzuri zaidi. Ninachoweza kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge ni kwamba utaratibu wa viza uliopo sasa hivi si kikwazo kwa biashara kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kufanya biashara katika nchi hizi mbili.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo kwa kutambua umuhimu wa kurahisisha zaidi tunatarajia kwamba amani itakapokuwa imetengemaa katika DRC mazungumzo yetu yatakamilika haraka ili tuweze kuwa na utaratibu mzuri zaidi.