Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Primary Question

MAGDALENA H. SAKAYA aliuliza:- Wilaya ya Kaliua inakabiliwa na tatizo kubwa sana la maji hali inayosababisha wananchi wake wengi kuteseka kwa kukosa huduma hiyo muhimu na kutumia muda mwingi kutafuta maji umbali mrefu na hivyo kushindwa kufanya shughuli za maendeleo. Je, mradi mkubwa wa kutoka Mto Malagarasi kwenda vijiji vya Kaliua mpaka Urambo utaanza lini na kukamilika lini?

Supplementary Question 1

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kumuuliza Mheshimiwa Waziri maswali mawili ya nyongeza.
Kwa kuwa huu ni mwaka wa nne tangu Serikali ilivyokuja na mpango wa kutoa maji Malagarasi lakini bado mradi uko kwenye upembuzi yakinifu na hata fedha iliyotengwa, shilingi bilioni mbili mwaka huu ni kwa ajili ya upembuzi yakinifu, wakati huohuo wananchi wa Kaliua wanaendelea kuteseka kupata maji na akina mama wanateseka na watoto hawaendi shule kwa wakati.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa huu ni mpango wa muda mrefu, Serikali ina mpango gani wa muda mfupi wa kuwapatia wananchi wa Kaliua maji ya uhakika na masafi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Kampuni ya GTI imefanikiwa kuchimba kisima cha maji kwenye Kata moja ya Usindi na ikapata maji mengi pamoja na kuwa ardhi ya Kaliua haina maji kwenye water table, Serikali sasa ina mpango gani wa kupeleka wataalam wenye uwezo mkubwa Kaliua waweze kugundua maeneo yenye maji ya uhakika kwenye ardhi ili angalau tupate visima vyenye maji ya kutosha wananchi wapate maji ya kutosha waache kuteseka na adha kubwa ya maji Jimbo la Kaliua? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza Mheshimiwa Sakaya alikuja ofisini na tukazungumza matatizo ya maji katika Wilaya yake na nikamueleza kwamba nitapeleka wataalam kupitia TUWASA ili wakasaidiane na Mhandisi wa Wilaya, inaonekana kidogo Mhandisi wa Wilaya hana uwezo wa kuweza kufanya usanifu wa miradi maana mpaka sasa ametengewa shilingi milioni 692 anataka azitumie zote kufanya usanifu, nimekataa kwamba haiwezekani ukatumia shilingi milioni 600 kwa usanifu, tunataka tupate matokeo.
Kwa hiyo, napeleka wataalam ili wakashirikiane angalau hata hicho kisima anachokizungumza tuweze kukiendeleza wananchi wa pale waweze kupata maji.(Makofi)