Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daniel Edward Mtuka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Mashariki

Primary Question

Mwasa MHE. DANIEL E. MTUKA aliuliza:- Kwa kuwa bwawa linalotarajiwa kuchimbwa katika Kijiji cha Mbwasa, Tarafa ya Kintinku ni bwawa la kimkakati kwa wakazi wa Tarafa nzima ya Kintinku. Je, ni lini Serikali itaanza rasmi ujenzi wa bwawa hilo baada ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kukamilika?

Supplementary Question 1

MHE. DANIEL E. MTUKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Nina maswali mawili ya ngongeza. Hali ya upatikanaji wa maji hasa katika eneo la Bonde la Ufa katika Jimbo la Manyoni Mashariki ni ngumu sana, hivi ninavyozungumza mifugo inahangaika, watu wanahangaika, akinamama wanalala kwenye visima ambavyo havina uhakika wa kupatikana kwa maji, hali ni ngumu sana kwa kweli. Mheshimiwa Waziri amejibu kwamba litawekwa katika kipaumbele cha bajeti inayokuja, ninaomba tu ni ombi, kwa emergency, kwa hali ambayo nimeielezea hii, hali ni ngumu, naomba liingizwe kwenye bajeti ya mwaka unaofuata.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, katika Kata ya Sorya Wilayani Manyoni, kwenye Jimbo langu katika harakati za kuhangaika kuwatafutia ajira vijana na akina mama tumetenga eneo, zaidi ya eka 400 kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na tumechimba visima vitatu kwa fedha yetu wenyewe. Tuna shida ya umeme kwa ajili ya kufunga pampu za kutoa maji ili tuweze kumwagilia.
Je, Serikali inaweza kutusaidia sasa kupeleka umeme kwenye visima vile ili kunusuru wananchi hawa wanaohangaika, hasa vijana, tuweze kumwagilia maeneo haya na tuweze kujinusuru kwa suala la njaa? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimhakikishie kama tulivyoji-commit kwenye jibu la msingi, kwamba tutaweka kwenye bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa hiyo naomba nimhakikishie kwamba tutafanya hivyo kwa sababu tumeshatoa jibu la namna hiyo.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu ekari 400 ambazo mmepanga kuendeleza kilimo cha umwagiliaji; nilipokee ombi lake lakini tutaangalia uwezo wa bajeti iliyotengwa kwa mwaka huu wa fedha, kama itawezekana tutasaidia, lakini vinginevyo tutaangalia katika bajeti ya mwaka utakaofuata.