Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. ELIAS J. KWANDIKWA aliuliza:- Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuboresha maeneo ya uendeshaji na usimamizi wa rasilimali ya Menejimenti, Bodi, Mabaraza ya Madiwani, Ukaguzi wa Nje, Ukaguzi wa Ndani na kuliacha eneo muhimu la Kamati za Ukaguzi (Audit Committee) kwenye Wizara, Idara, Wakala na Serikali za Mitaa. Je, ni lini Serikali itaboresha Kanuni ili muundo wa Kamati za Ukaguzi ziundwe na Wajumbe wengi (majority) toka nje ya taasisi kuzingatia weledi na uzoefu ili kusimamia rasilimali kwa tija na ufanisi?

Supplementary Question 1

MHE. ELIAS J. KWANDIKWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Naipongeza sana Serikali kwa hatua inayochukua ili kuweza kuboresha usimamiaji wa rasilimali zetu.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa uwepo wa Kamati za Ukaguzi ni muhimu sana katika kuimarisha mfumo wa udhibiti katika taasisi hususan katika Halmashauri zetu. Kwa kuwa Kamati imara husaidia Maafisa Masuuli kutimiza wajibu wao na hii Kamati ni muhimu kwa ajili ya kusimamia pia mpango kazi wa Wakaguzi wa Ndani na Wakaguzi wa Nje. Kwa kuwa Serikali imetoa mwongozo wa mwaka 2013 na haujatekelezwa vizuri katika Halmashauri zetu.
Je, Serikali iko tayari kuzielekeza upya Halmashauri zetu kutekeleza mwongozo huu mzuri kikamilifu ili kuleta tija zaidi katika usimamiaji wa rasilimali zetu? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wake katika kuhakikisha rasilimali za Taifa letu zinatumika ipasavyo na kama ailivyouliza, sisi kama Wizara tupo tayari na tumekuwa tukihakikisha Kamati hizi zinatekeleza maelekezo na miongozo yote inayotolewa na Wizara ya Fedha.
Mheshimiwa Spika, sasa kama nilivyosema katika jibu langu la msingi kwamba tunaendelea kushughulikia sheria hii pamoja na kanuni zake ili tuje na sheria itakayohakikisha rasilimali za Taifa letu zinasimamiwa ipasavyo.