Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Mohamed Chuachua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Primary Question

MHE. RASHID M. CHUACHUA aliuliza:- Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zinazopoteza fedha nyingi kwa ajili ya misamaha ya kodi ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kigezo cha kuvutia wawekezaji na katika hotuba ya Bajeti 2013/2014 ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Mheshimiwa William Mgimwa alisema misamaha ya kodi kwa mwaka 2011/2012 ilifikia asilimia 4.3 ya pato la Taifa:- (a) Je, hali ya misamaha ya kodi ikoje kwa sasa ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011/2012? (b) Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Mwaka 2009/2010 Tanzania ilipoteza asilimia 15 ya pato lililotarajiwa kukusanywa iwapo misamaha isingetolewa, 2010/2011 asilimia nane na kwa mwaka wa 2011/2012 asilimia 27; je hali ya misamaha ikoje kuanzia mwaka 2013/2014 hadi sasa.

Supplementary Question 1

MHE. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba niulize swali moja la nyongeza. Ni kweli kuwa si kila msamaha wa kodi una madhara katika jamii na uchumi, hata hivyo ipo misamaha ya kodi isiyo na tija. Kwa kuwa hadi kufikia mwaka 2015/2016 misamaha ya kodi ilifikia asilimia 8.6 ya mapato yote ya kodi. Mpango wa Serikali ni upi kuhusu misamaha ya kodi kwa mwaka wa fedha 2017/2018? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ameuliza mpango wa Serikali kwa mwaka huu. Naomba nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali sasa hivi iko katika mchakato wa kuangalia tax measures itakayohusishwa na misamaha ya kodi kwa mwaka huu. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge awe na subira, tarehe nane ni keshokutwa, Serikali yetu italeta mapendekezo yote na Bunge lako Tukufu litapitisha hayo mapendekezo ya Serikali. (Makofi)