Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Tanzania imejaaliwa kuwa na almasi na madini ya aina mbalimbali kwa wingi ikiwemo gypsum; (a) Je, ni busara kwa viwanda vyetu humu nchini kuagiza gypsum kutoka nje ya nchi? (b) Je, Serikali haioni kuwa huo ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za Watanzania?, na (c) Serikali inachukua hatua gani kukomesha utaratibu huu ili kutunza fedha zetu chache za kigeni na kulazimisha ajira kwa Watanzania katika machimbo ya gypsum hususan Itigi?

Supplementary Question 1

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa madini haya ya jasi
(gypsum) yako mengi sana katika nchi hii hasa Itigi, Msagali maeneo ya Mpwapwa na maeneo mengine. Baadhi ya nchi ambazo zinatuzunguka hazina madini haya ya jasi ikiwemo Congo, Rwanda na Burundi. Je, Serikali itasaidiana na wajasiriamali na wachimbaji wadogo hawa wa jasi kuwapatia masoko katika nchi hizi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa viwanda vya cement vinatumia malighafi hii ya jasi kutengenezea cement lakini sasa kuna baadhi ya viwanda ambavyo vimewekezwa nchi hii vinaagiza clinker moja kwa moja kutoka nchi za Ulaya na Asia. Je, Serikali sasa iko tayari kuhakikisha viwanda vya cement ambayo vitawekwa baadaye vinafanya processing hapa hapa nchini ikiwemo kujenga matanuru ambayo jasi itatumika? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Answer

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, kuhusu kusaidia wawekezaji waweze kutosheleza viwanda vya ndani na ku-export jasi hiyo ni sehemu ya shughuli yangu. Mheshimiwa Mbunge tutakutana tuwa-organize vijana tuweze kuwaongoza kwenda sokoni. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu kuagiza clinker kutoka nje napenda niliambie Bunge lako Tukufu kwamba, uwezo uliosimikwa wa viwanda vya Tanzania vyenye uwezo wa kuzalisha cement tani milioni kumi na laki nane kwa mwaka tuna uwezo wa kujitosheleza clinker. Hata hivyo, jambo moja la kufurahisha, wenye viwanda vyote 11 walikutana Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Dkt. Meru, Katibu Mkuu wangu na wakakubaliana wao kwamba watapeana clinker yenye viwango na yenye bei nzuri. Hakuna haja ya kuagiza nje wakati clinker inapatikana hapa.