Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hassan Elias Masala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nachingwea

Primary Question

MHE. HASSAN E. MASALA aliuliza:- Huko Nachingwea kulikuwa na viwanda viwili vya kukamua ufuta na korosho ambavyo vimebinafsishwa kwa muda mrefu lakini wawekezaji hawajaviendeleza hadi sasa hivyo kupunguza ajira na mzunguko wa fedha:- (a) Je, Serikali ina mpango gani juu ya wawekezaji waliopewa viwanda hivyo viwili? (b) Kama wawekezaji hao wameshindwa kuendeleza viwanda hivyo, je, Serikali ina mpango gani na viwanda hivyo hasa ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeonesha nia ya kufufua viwanda nchini?

Supplementary Question 1

MHE. HASSAN E. MASALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Naomba kwanza nitambue jitihada ambazo Serikali imefanya kwa kuona umuhimu wa kufufua viwanda hivi Naomba niulize maswali yafuatayo.
Mheshimiwa Spika, mkataba umesainiwa Machi, 2017 na tunategemea kufanya uzalishaji mwezi Septemba mwaka huu, takribani itakuwa miezi tisa. Naomba nifahamu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, mpaka sasa hivi taarifa nilizonazo ndani ya kiwanda kile kuna mashine zisizopungua 30 zimeshawekwa na mashine hizi ni za manual (za mikono). Sasa nataka nijue mashine hizi ni hii Kampuni ya Sunshine ambayo imeingia mkataba au ni watu wengine ambao wamezileta hizi mashine? Muhimu nilikuwa nataka nijue ambao watu wa Nachingwea wanaufanya.
Mheshimiwa Spika, lakini swali lingine sambamba na hilo, nataka nipate majibu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, majengo ya kiwanda kile cha korosho mpaka sasa hivi yako chini ya Lindi Pharmacy na yanatumika kama maghala ya kuhifadhia korosho. Je, kiwanda hiki ambacho Wachina wamefanya mkataba nacho ni kiwanda gani ambacho kinaenda kujengwa na kinaenda kujengwa maeneo gani?Au ni majengo yale yale yatatumika?

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Answer

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, napenda nikiri, maswali aliyoniuliza ni undani wa MOU na mimi sijaisoma. Kwa hiyo, nitakwenda kwenye MOU niweze kujua undani wa nani anamiliki nini na nani atapata nini.