Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hamidu Hassan Bobali

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mchinga

Primary Question

MHE. HAMIDU H. BOBALI aliuliza:- Gereza la Kingulungundwa lililopo Wilayani Lindi linakabiliwa na uhaba mkubwa wa Nyumba za Askari na miundombinu mibovu:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha makazi ya Askari katika Gereza hilo? (b) Gereza hili lipo umbali wa kilometa tatu kutoka barabara kuu inayotoka Dar es Salaam kwenda Lindi, lakini wakati wa masika, barabara hiyo haipitiki kwa gari kutokana na kujaa tope na maji. Je, Serikali haioni kuwa kukosekana kwa mawasiliano ya barabara kutoka Gerezani ni jambo la hatari?

Supplementary Question 1

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, lakini majibu aliyonijibu ni too general. Mimi niliulizia suala la Kingulungundwa lakini ametoa takwimu nyingi za Magereza ya Ukonga na maeneo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza la nyongeza; nahitaji kufahamu hizi nyumba 320 ambazo Mheshimiwa Waziri amezisema zinajengwa huko Ukonga na maeneo mengine; je, kati ya hizo, Kingulungundwa zinapelekwa nyumba ngapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Gereza lile, kuna shida kubwa ya maji ambayo inasababisha wakati mwingine wafungwa na Askari watumie muda mwingi kabisa kutafuta maji. Kama inavyofahamika, hili ni Gereza maalum kwa Mkoa wa Lindi, limewekwa mbali kidogo na makazi ya wananchi kwa kazi maalum ambayo nadhani Mheshimiwa Waziri anaijua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba kupata commitment ya Mheshimiwa Waziri ni lini Serikali itawapatia maji Gereza la Kingulungundwa na jirani zao wa Mjimwema ili kuondoa adha ambayo wanaipata wafungwa na Maafisa wa Gereza lile? (Makofi)

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Bobali, Goal Keeper wa Timu ya Bunge ya Wabunge wa Yanga, kama ifuatavyo:- (Makofi)
Moja, suala la nyumba za Ukonga; tulikuwa tunaelezea tu commitment ya Serikali kuhusu nyumba za Askari Magereza kwa maana ya kwamba zinajengwa kule, tunaendeleza ili kutatua tatizo hilo na tunakamilisha nyumba nyingine ambazo ziko katika hatua za mwisho ili Askari waweze kuhamia, hatuzihamishi zile za Ukonga kwenda Gereza lile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu upande wa maji,
hata wakati napitisha bajeti, Mheshimiwa Salma Kikwete aliniambia hatashika shilingi, lakini anaomba siku nikipita Lindi niende kwenye Gereza hilo kujionea tatizo hilo la maji. Mheshimiwa Mbunge amelitaja jambo hili, naweka uzito, nitakapozungukia kule, nitahakikisha napita kujionea lakini hoja hiyo tumeshaipokea kama Serikali kuhakikisha kwamba tunaweka kipaumbele kuweza kuhakikisha kwamba suala la maji linaenda sambamba na hilo la barabara ambalo lilikuwepo kwenye swali la msingi. (Makofi)

Name

Eng. Atashasta Justus Nditiye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. HAMIDU H. BOBALI aliuliza:- Gereza la Kingulungundwa lililopo Wilayani Lindi linakabiliwa na uhaba mkubwa wa Nyumba za Askari na miundombinu mibovu:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha makazi ya Askari katika Gereza hilo? (b) Gereza hili lipo umbali wa kilometa tatu kutoka barabara kuu inayotoka Dar es Salaam kwenda Lindi, lakini wakati wa masika, barabara hiyo haipitiki kwa gari kutokana na kujaa tope na maji. Je, Serikali haioni kuwa kukosekana kwa mawasiliano ya barabara kutoka Gerezani ni jambo la hatari?

Supplementary Question 2

MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Gereza kuu la Wilaya ya Kibondo pamoja na kuhudumia Watanzania na mahabusu kwa wafungwa, linahudumia vile vile mahabusu na wafungwa kutoka nchi jirani ya Burundi kwa maana ya Wakimbizi kwa wingi sana. Lina upungufu mkubwa sana wa maji na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la UNHCR liliahidi kwamba litasaidia kuleta mradi wa maji kwa Gereza lile na taarifa tulishazitoa mpaka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Je, Srikali imefikia hatua gani kuwalazimisha sasa wale watu wa UNHCR walete maji katika Gereza hilo la Kibondo? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nampongeza Mheshimiwa Nditiye kwa kufuatilia jambo hili na mara kwa mara tukionana, amekuwa akinikumbushia jambo hili hili. Nimwambie tu kwamba, kati ya wiki hii mpaka wiki ijayo, timu ya Wawakilishi wa Shirika la Wakimbizi Duniani hapa kwetu nchini, pamoja na wadau wanaoshughulikia masuala ya wakimbizi, watazungukia Mkoa wa Kigoma, watazungukia makazi likiwemo Gereza hilo na moja ya ajenda kubwa wanayokwenda kufanya ni kuangalia miundombinu jinsi inavyoweza kusaidia uwepo wa watu wengi katika Makambi pamoja na Magareza kama hilo ambalo amelitaja.