Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Kuna maeneo ambayo hayana kabisa mitandao ya mawasiliano huko Mpanda Vijijini hususan kata ya Katuma, Sibwesa, Mwese na maeneo ya Bujumbo, Kapanda pamoja na Wilaya ya Mlele kata ya Ilunde. Je, ni lini Serikali itawapelekea mawasiliano wananchi wa maeneo hayo?

Supplementary Question 1

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mawasiliano sasa hivi kwa wananchi ni uchumi. Kwa sababu wananchi sasa hivi wanafanya mawasiliano kwa mambo mengi ya kibiashara ya mawasiliano ya magonjwa na kila kitu na vilevile mawasiliano ninafikiri kama hakuna sehemu hakuna mawasiliano hakuna maendeleo. Katika kata za Sibwesa na Kasekese wameweka minara tayari toka Mei na pesa zimashatumika sasa ni lini Serikali itawasha kwa sababu wananchi wanaona ile minara lakini haina faida katika muono wao?
Swali la pili, wananchi wa Ilunde wameahidiwa kwa muda mrefu sana kuhusu mawasiliano. Na ukiangalia kata ya Ilunde iko katikati ya pori ina maana wananchi wale maisha yao yako hatarishi na wengine wanakwenda kupanda kwenye miti, wengine wanadondoka wanavunjika mikono na miguu kwa ajili ya kutafuta mawasiliano. Ninaomba kauli ya Serikali, ni lini sasa Serikali itawajengea mnara kata ya Ilunde? (Makofi)

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana kabisa na Mheshimwa Mbunge kwamba mawasiliano ni biashara na nakubaliana naye kwamba ni muhimu sana kuwe na mawasiliano maeneo yote na kama nilivyosema katika majibu yangu ya swali la msingi kwamba Serikali nia ya dhati ya kuhakikisha tunapeleka mawasiliano kila sehemu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naomba nikiri kwamba mikoa mitatu hii ya Songwe, Rukwa na Katavi sijaizungukia sawa sawa ili nijue hasa matatizo yake katika sekta zote tatu. Nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba baada ya kikao hiki cha Bunge la Bajeti nitafika katika mikoa hii mitatu hususan katika kijini hiki cha Ilunde nione na nipate hali halisi. Na mimi nijisikie haliā€¦na hatimaye tupange mipango ya kuondoa matatizo haya.

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Kuna maeneo ambayo hayana kabisa mitandao ya mawasiliano huko Mpanda Vijijini hususan kata ya Katuma, Sibwesa, Mwese na maeneo ya Bujumbo, Kapanda pamoja na Wilaya ya Mlele kata ya Ilunde. Je, ni lini Serikali itawapelekea mawasiliano wananchi wa maeneo hayo?

Supplementary Question 2

MHE. ABDALLAH H. ULEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa rufsa hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo haya yaliyopo kwenye Mkoa wa Katavi yako pia katika imo jimbo langu la Mkururanga kilometa 60 tu kutoka katika Mkoa wa Dar-es salaam ambapo kata za Kwanzuo Kisegese, Mkamba na kwingineko ikiwa ni pamoja na kijiji ambacho wewe unalima kijiji cha Koragwa Tundani na pale Mkuranga maeneo ya Kiguza. Yote yana shida ya mawasiliano.
Je, Mheshimiwa Naibu yuko tayari yeye na hao viongozi wa huo Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kushirikiana name kuhakikisha maeneo haya yanapata mawasiliano? (Makofi)

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli kwa dhati kabisa niko tayari.

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Kuna maeneo ambayo hayana kabisa mitandao ya mawasiliano huko Mpanda Vijijini hususan kata ya Katuma, Sibwesa, Mwese na maeneo ya Bujumbo, Kapanda pamoja na Wilaya ya Mlele kata ya Ilunde. Je, ni lini Serikali itawapelekea mawasiliano wananchi wa maeneo hayo?

Supplementary Question 3

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona niulize swali ndogo la nyongeza. Matatizo ya usikivu wa simu yaliyopo Mpanda vijijini ni sawa na yaliyopo Wilaya ya Ngara kata Muganza, Nyakisasa Keza, Kabanga na Rusumo. Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha usikivu wa simu katika kata hizo?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema Serikali ina nia ya dhati kabisa yakufikisha mawasiliano kila sehemu na hasa, eneo hili analoliongelea ni maeneo ya mpakani na maeneo ya mpakani tuna utaratibu maalum wa kuhakikisha kwamba mawasiliano yanafika haraka katika maeneo hayo. Kwa hiyo Serikali itahakikisha inafikisha mawasiliano mara fedha zitakapozipata.

Name

Anna Joram Gidarya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Kuna maeneo ambayo hayana kabisa mitandao ya mawasiliano huko Mpanda Vijijini hususan kata ya Katuma, Sibwesa, Mwese na maeneo ya Bujumbo, Kapanda pamoja na Wilaya ya Mlele kata ya Ilunde. Je, ni lini Serikali itawapelekea mawasiliano wananchi wa maeneo hayo?

Supplementary Question 4

MHE. ANNA J. GIDARYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Matatizo yaliyoko Katavi yanafanana sana na matatizo yaliyoko katika Jimbo la Babati Vijijini kata ya Duru vijiji vya Endagwe, Hoshan, Ameyu, Eroton na Wikanzi maeneo haya hayana mawasiliano ya simu. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri ni lini maeneo haya yatapewa vipaumbele ukizingatia uwanja wa ndege wa Manyara unapelekwa Mwikanzi?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, mara tutakapopata fedha tutahakikisha tunapeleka mawasiliano katika maeneo haya ya Mkoa wa Manyara na hasa maeneo hayo ambayo tuna kusudia kujenga uwanja wa ndege kama ambavyo Mheshimiwa Anna umeyaeleza.