Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Issa Ali Abbas Mangungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. ISSA A. MANGUNGU aliuliza:- Wazee wa Mabaraza katika Mahakama Kuu hasa Dar es Salaam husikiliza kesi zinazohusu mauaji na kulipwa sh. 5,000:- Je, Serikali haioni ni wakati muafaka sasa kuwaongezea posho wazee hao?

Supplementary Question 1

MHE. ISSA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kama Serikali inatenga bajeti, je, Mheshimiwa Waziri anajua kwamba Wazee wa Baraza wanakopwa na hawalipwi kwa wakati posho zao na wengine mpaka wanafikia kukutwa na umauti wakiwa wanadai pesa nyingi sana idara ya mahakama, je, hilo analitambua?
Mheshimiwa Spika, lakini la pili, kwa posho ya sh. 5,000
na uzito wa kesi wanazoamua wazee hawa hamuoni kwamba Serikali yenyewe inachochea vitendo viovu vya rushwa na mambo mengine katika mahakama zetu katika kutoa maamuzi? (Makofi)

Name

Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilosa

Answer

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, ni kweli yapo malimbikizo ya posho ya Wazee wa Baraza na mpaka sasa malimbikizo hayo ni sh. 335,479,000; na tunatarajia kwa fedha ambayo imetengwa mwaka huu kuweza kulipa malimbikizo hayo ya fedha hizo wanazodai Wazee Wa Baraza.
Mheshimiwa Spika, pia tunatambua kabisa kwamba kiwango cha sh. 5,000 kwa mazingira ya leo ni kiasi kidogo ndiyo maana Serikali na Mahakama inafanya jitihada ya kuona uwezekano wa kuongeza posho hiyo, sio tu kwa Wazee wa Baraza wa Dar es Salaam bali Wazee wa Baraza wa Mahakama zote nchini.