Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. ALMAS A. MAIGE (K.n.y. MHE. MUSA R. NTIMIZI) aliuliza:- Eneo la kilometa 89 la kipande cha Barabara ya Chaya – Nyahua katika Barabara ya Itigi – Chaya – Nyahua -Tabora bado halijaanzwa kutengenezwa:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kujenga kipande hicho kwa sababu kwa sasa hakipitiki kabisa? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kipande hicho kinapitika wakati wote wakati mchakato wa ujenzi wa barabara hiyo ukiendelea?

Supplementary Question 1

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Barabara hii ambayo sasa hivi iko chini ya plan ya kujengwa kwa kiwango cha lami imekuwa na matatizo sehemu zile za Kizengi ambako madaraja yake ni mabovu na ikitokea dharura yoyote gari moja likazimikia barabarani magari mengine hayapiti. Je, katika kipindi hiki cha kungojea Serikali ina mpango gani wa kupanua Daraja lile la Kizengi?
Mheshimiwa Spika, pili, barabara hii inaunganisha Mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora lakini hatuoni uharaka wa kujenga barabara hii. Je, Serikali sasa inaweza kutuambia ni lini hasa ujenzi huu utaanza?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Almas Maige kwamba tulichokisema, ile sentensi ya mwisho, kwamba TANROADS itaendelea kuifanyia matengenezo barabara hii ili iweze kupitika majira yote hii ni pamoja na madaraja. Kwa hiyo, asiwe na wasiwasi, matengenezo haya yanahusisha na madaraja.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili, nimhakikishie kwamba taratibu tumezianza na tutaanza kujenga hii barabara mara baada ya kukamilika evaluation na tukampata mkandarasi.