Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kunti Yusuph Majala

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KUNTI Y. MAJALA (K.n.y. MHE. PAULINE P. GEKUL) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la ulipaji wa ushuru wa huduma ambao ni asilimia 0.3 unaotozwa kutoka mitandao ya simu ambao kwa sasa Halmashauri zimeshindwa kukusanya ipasavyo?

Supplementary Question 1

MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri, ni masuala yale yale kwamba tupo kwenye mchakato. Naomba kupata majibu katika maswali yangu mawili.
(a) Ni lini sasa TAMISEMI itakamilisha mchakato wa marekebisho ya sheria hiyo ili Halmashauri zetu ziweze kujipatia mapato yake stahiki?
(b) Ni lini kikao hicho cha wadau kitakwenda kufanyika ili tuweze kuokoa mapato mengi yanayopotea katika sekta hii? Asante.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kwamba ni kweli kumekuwa na kero kwa Waheshimiwa Wabunge wote katika Majimbo yote kwa sababu minara imeenea maeneo yote.
Mheshimiwa Spika, kila mtu katika Jimbo lake ana mnara na kila mtu anatarajia kukusanya kodi. Lengo ni kuhakikisha Halmashauri zinapata mapato, ndiyo maana ofisi yetu imeona, kwa sababu suala hili linagusa Halmashauri zote, lazima tuwe na mfumo ambao utakuwa muafaka kuhakikisha kwamba fedha zinakusanywa hali kadhalika Halmashauri zinapata fursa ya kukusanya hayo mapato vizuri na ndiyo maana mchakato huo umeshaenda.
Mheshimiwa Spika, bahati nzuri sana kikao cha wadau kimeshakamilika, na jukumu linalofanyika ni kwamba paper itaondoka katika Baraza za Mawaziri, itajadiliwa na itakuja huko. Hata hivyo, tumeenda mbali katika marekebisho ya sheria hii, tunaenda kuangalia suala zima la crop cess, watu wanajua ushuru wa mazao umekuwa ni changamoto kubwa sana.
Kwa hiyo, sheria hii inakutanisha mambo mengi ili mradi Sheria ya Fedha Sura Namba 290 itakapokuja hapa Bungeni, basi iweze kukidhi mahitaji ya Waheshimiwa Wabunge wote katika Halmashauri zao, fedha ziweze kukusanywa na wananchi wapate huduma bora. Asante.