Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Martha Jachi Umbulla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARTHA J. UMBULLA Aliuliza:- Kulingana na takwimu za mwaka 2010 Mkoa wa Manyara unaongoza kwa mila potofu ya ukeketaji wa wanawake kwa asilimia 71 hapa nchini hali inayotisha na kuhatarisha maisha ya wanawake. (a) Je, Serikali katika kufanya utafiti imebaini ni Wilaya zipi na vijiji vipi vinaongoza? (b) Je, hali hii na mila hii potofu imesababisha athari na vifo kiasi gani mkoani Manyara? (c) Je, Serikali ina mikakati gani ya dharura ya kukabiliana na mila hii potofu ili kuondoa kabisa athari za ukeketaji?

Supplementary Question 1

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, kwanza nachukua nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa juhudi yake kubwa, amekuja mara nyingi katika Mkoa wetu wa Manyara kutatua kero mbalimbali za wananchi hasa katika sekta ya afya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naomba kutoa masikitiko yangu kwamba sijaridhika na majibu ya Serikali katika swali langu hili la namba 94.
Kama tatizo liko kwa asilimia 100 katika mkoa, ina
maana kwamba lazima kwa utafiti uliofanywa na Serikali kuna vigezo vilivyoonyesha kwamba lazima kuna takwimu ambazo zinaonyesha asilimia 100 imetokana na vitu gani, hasa vifo na adhari mbalimbali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu (b) ya swali langu nilitaka kupata idadi ya vifo, siyo sababu zinazosababishwa na ukeketaji kwa sababu hizo tunazijua. Nilitaka kupata takwimu ni vifo kiasi gani na maeneo gani ili sisi viongozi wa Mkoa wa Manyara tuweze kupambana, tuongeze juhudi ya
Serikali kapambana na janga hili ambalo liko kwa asilimia 100 katika mkoa wetu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, nini kauli ya Serikali kufuatana na hali hii mbaya katika mkoa wetu wa Manyara?
Swali la pili, kwa maelezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri, amesema tunatumia Maafisa Maendeleo ya Jamii na Afisa Ustawi wa Jamii ili kutoa elimu kupambana na janga hili, lakini Maafisa Maendeleo ya Jamii na Afisa Ustawi wa Jamii wako siku zote na hali imefikia asilimia 100.
Sasa je, Serikali ina mikakati gani ya ziada ili kupambana na tatizo hili specifically kwa Mkoa wa Manyara ili na sisi Manyara tubaki salama?

Name

Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Namshukuru Mheshimiwa Martha Jachi Umbulla, kwa maswali yake ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu yetu ni kwamba
kwanza, asilimia 100 siyo kwamba ni watu wote. Ni kwamba tatizo hili lipo zaidi Vijijini kuliko maeneo ya Mijini, lakini kiwango hasa cha kitakwimu kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na
National Bureau of Statistics ni kwamba katika wanawake 100 wa Mkoa wa Manyara, basi wanawake 71 wamekeketwa. Idadi ya vifo hatukuweza kupata takwimu za idadi yake kwa
uhakikika kwa sababu vitendo vya ukeketaji vinafanyika gizani, vinafanyika kwa siri na utamaduni umebadilika, badala ya kuwakeketa kipindi kile cha usichana mdogo, sasa hivi wanakeketa watoto wachanga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna mbinu mpya
ambayo wamegundua, wanawakeketa watoto wakati wakifanya tohara kwa watoto wa kiume. Kwa hiyo, wanawachanganya, inakuwa kama ni sherehe ya tohara inayokubalika kisheria kwa watoto wa kiume wanawaunganisha na watoto kike. Kwa hiyo, kuna mbinu nyingi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika kujibu maswali yake, najibu tu yote kwa pamoja mawili kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza hapa, aligusia Legal Anthropology. Sisi kwenye tiba tunazungumzia Medical Anthropology, sasa tunapo-approach tatizo pamoja na kuwa na sheria, pamoja na kuwa na mambo mengine, hatuwezi kujikita kwenye sheria peke yake, ni lazima tuitazame jamii nzima holistically, lazima tuitazame jamii nzima kwa ujumla wake. Tuzitazame mila na desturi za jamii husika, tutazame namna ya kupenya kwenye hiyo jamii ili kuufikisha ujumbe wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa msingi huo, tumekuja na mkakati mpya sasa wa kutumia mbinu inaitwa kwamba alternative right of passage. Kwa sababu kwenye mila za kukeketa, imebainika kwamba ni lazima zifanywe na jamii
zinazofanya mambo hayo kwa sababu wanataka kuwagraduate watoto wa kike kutoka kwenye status ya usichana na kwenda kwenye status ya uanamke. Sasa kama wasipokeketwa, wanaume wanakataa kuwaoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ili ku-address hili tatizo, huwezi kutumia sheria peke yake, ni lazima uelewe sababu hizo na sasa mbinu yetu mpya ya ARP (Altenative Right of Passage) tunaitumia kwa maana ya kuyafikia viongozi
wa kimila na watu mashuhuri kwa jamii husika ili kufikisha ujumbe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo namshauri Mheshimiwa Martha Umbulla na viongozi wote wa kimila na Kiserikali katika Mkoa wa Manyara kuanza kuhamasisha jamii yao kuachana na mila hizi kwa hiari na kwa kuwaelewesha kuliko kutumia zaidi nguvu. Ahsante.