Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE (K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA) Aliuliza:- Je, kwa nini Serikali haitumii mfumo wa Ubia na Sekta Binafsi (PPP) kwenye mipango yake ya ununuzi wa vifaa tiba vya bei kubwa kama MRI, CT-Scan na X-Ray?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipatia fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Naipongeza Serikali kwa mtazamo huo mpya na ninaamini sasa huo ndiyo mtazamko chanya ambao tunapaswa kwenda nao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa sasa hivi katika ununuzi wa vifaa tiba tumekuwa tukivinunua bila kuwa na mpango wa matengenezo kwa maana ya Plan Preventive Maintenance, kuwekwa katika mpango wa
manunuzi.
Je, sasa Serikali mtakuwa tayari kuhakikisha wakati mna-negotiate kununua zile mashine mnaweka mpango wa Preventive Maintenance kwa sababu sasa hivi gharama zinazotumika kutengeneza vifaa tiba ni za juu sana?
Swali la pili, kwa kuwa, gharama za utengenezaji wa vifaa hivi ni kubwa sana, kwa maana ya
Preventive Maintenance na pale vinapokuwa vinaharibika kwa hali ya kawaida:-
Je, Serikali haioni sasa ni muda muafaka kuingiza gharama za PPM ama Plan Preventive Maintenance katika gharama za vitendanishi, badala ya kutenga peke yake ambazo ni mabilioni ya hela ambapo mara nyingi Serikali inaishia kutozilipa?

Name

Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inakubaliana na wazo lake kwamba gharama za Planned Preventive Maintenance ni vema zikawa sehemu ya mkataba mkuu wa ununuzi wa vifaa tiba. Hivyo, ndiyo maana mikataba yote mipya ambayo itafungwa na Serikali na Private Contractors kwa sasa itahuisha uwepo wa section maalum ambayo ina Planned Preventive Maintenance katika costs zake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili pia tunakubaliana naye kwamba ni lazima tuziingize gharama za PPM kwenye manunuzi ya vitendanishi. Pia tunakubaliana naye kwamba ni wazo zuri, naomba nilichukue na nitalifanyia
kazi ndani ya Serikali.