Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Primary Question

MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJAD aliuliza:- Kituo cha Polisi Maruhubi kinakabiliwa na matatizo mbalimbali kama vile ukosefu wa askari wa kutosha; kituo hakitoi huduma saa 24, lakini pia majengo yake ni machakavu sana kiasi kwamba hayana hadhi ya kuwa Kituo cha Polisi:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka askari wa kutosha katika kituo hicho na kuhakikisha kuwa kituo kinatoa huduma zake kwa saa 24? (b) Je, ni lini Serikali itayakarabati majengo ya kituo hicho ili yaendane na hadhi ya Kituo cha Polisi?

Supplementary Question 1

MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJAD: Mheshimiwa Spika, napenda kuuliza swali moja la nyongeza. Je, ni lini watapata fedha na ukarabati wa kituo hicho kwa sababu, eneo hili ni maarufu na lina matatizo sana ya huduma za kipolisi?
Kwa hiyo, kutoa nafasi kwa saa 12 tu haitoshelezi kwa sababu, kuna maeneo mengi ya uhalifu na historia inaonesha na ripoti zipo, lakini muda unakuwa ni mchache ambapo wananchi wakihitaji huduma za kipolisi wanashindwa kuzipata mpaka wazifuate sehemu za mbali na uhalifu unakuwa umeshatendeka. Je, Mheshimiwa Waziri haoni umuhimu kukipa kipaumbele kituo hiki kwa bajeti hii?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ussi Pondeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Kituo cha Maruhubi kinafungwa saa 12.00 jioni siyo kwa sababu ya ukosefu wa fedha, lakini kwa mujibu wa taratibu kulingana na Police General Order (PGO) Namba 287(9) inaeleza utaratibu wa vituo vya polisi vilivyo; kuna class A, B na C. Kwa hiyo, Kituo cha Maruhubi ni Class C ambacho kwa kawaida kinapaswa kifunguliwe saa 12.00 na kifungwe saa 12.00 jioni.

Name

Masoud Abdalla Salim

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mtambile

Primary Question

MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJAD aliuliza:- Kituo cha Polisi Maruhubi kinakabiliwa na matatizo mbalimbali kama vile ukosefu wa askari wa kutosha; kituo hakitoi huduma saa 24, lakini pia majengo yake ni machakavu sana kiasi kwamba hayana hadhi ya kuwa Kituo cha Polisi:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka askari wa kutosha katika kituo hicho na kuhakikisha kuwa kituo kinatoa huduma zake kwa saa 24? (b) Je, ni lini Serikali itayakarabati majengo ya kituo hicho ili yaendane na hadhi ya Kituo cha Polisi?

Supplementary Question 2

MHE. MASOUD ABDALLA SALIM: Mheshimiwa Spika, na mimi nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri katika jibu la muuliza swali la msingi (b) alieleza kwamba yuko tayari kukarabati kituo cha polisi husika ambacho kimetajwa, lakini kituo cha polisi cha Kengeja ni kibovu, chakavu, kinavuja na kuta zake zimeanza kudondoka na ni athari sana kwa polisi na kituo hicho mmerithi kutoka kwa wakoloni.
Je, hamuoni kwamba ni aibu na fedheha kwamba hamuwezi kukikarabati na inawezekana kikapelekea askari hawa kupoteza maisha? Hamuwezi kukarabati hata lile ambalo mmerithi kwa wakoloni!?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nakiri kabisa kwamba kituo cha Kengeja hali yake siyo nzuri, hata mimi niliwahi kufanya ziara pale, lakini siyo Kengeja tu, ni maeneo mengi ndani ya nchi yetu vituo vya polisi haviko vizuri sana. Kwa mfano, Mkoani ni zaidi! Nadhani Kituo cha Mkoani kina hali mbaya zaidi kuliko Kengeja.
Mheshimiwa Spika, kama alivyozungumza mwanzo Mheshimiwa Mbunge, ni kwamba tuna mkakati wa kuvifanyia ukarabati vituo hivi na utaratibu huo utakuwa unaenda hatua kwa hatua kulingana na hali ya fedha itakavyoruhusu. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Masoud uvute subira.