Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA Aliuliza:- Pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kutatua matatizo ya wakulima wa tumbaku katika Mkoa wa Tabora akiwemo wa Wilaya ya Urambo. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuunda Bodi ya Tumbaku (TTB) nyingine ili ianze kazi haraka iwezekanavyo baada ya Bodi ya Tumbaku iliyovunjwa? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha pembejeo za msimu ujao zinamfikia mkulima wa tumbaku mapema wakati huu ambapo bodi husika imevunjwa?

Supplementary Question 1

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu. Pamoja na majibu yako na jitihada kubwa inayochukuliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu katika kutatua changamoto za zao la tumbaku, naomba niulize maswli ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, msimu wa kuuza tumbaku, yaani msimu wa masoko ya tumbaku ni sasa, ni mwezi huu wa nne, Serikali inatoa kauli gani kuhusu yafuatayo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza uongozi wa AMCOS ambao umefutwa kutokana na agizo la Serikali na kuwaacha bila uongozi kipindi hiki ambacho masoko yanaanza? Serikali inasema nini kuhusu suala hili? Ikiwemo AMCOS ya Utenge na Nsenga ambazo hazina uongozi hadi
sasa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali
inasemaje kuhusu kuwasaidia wakulima ambao
wamejitahidi wao wenyewe kutokukopa, lakini hatimaye wamejikuta wanabebeshwa madeni yasiyowahusu na kuwaacha hoi kiuchumi. Serikali inatoa kauli gani? Ahsante.

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uuzaji wa tumbaku katika mazingira ambayo uongozi wa AMCOS umefutwa au umesimamishwa; taratibu zitaendelea kushughulikiwa kwa kupitia Chama Kikuu katika maana hiyo WETCU na kama nilivyokwishsema tayari WETCU imewekewa utaratibu wa mpito, ili kuweza kufanya kazi zake kama kawaida. Kwa hiyo, kama kuna AMCOS ambazo hazina uongozi uuzaji wa tumbaku utaendelea kushughulikiwa na chama kikuu cha
ushirika, lakini vilevile kwa kushirikiana na vyombo vingine kama Maafisa Ushirika, lakini vilevile kwa kupitia watendaji ambao bado wapo kwenye Bodi ya Tumbaku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Mheshimiwa Mbunge ameuliza kuhusu wakulima ambao wanalazimika kubeba mzigo wa madeni ambayo yametokana na wao kuwepo kwenye vyama vya ushirika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kati ya sababu zilizosababisha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuchukua maamuzi mazito kuhusiana na WETCU na Bodi ya Tumbaku ni kwa sababu kulikuwa na usimamizi mbovu sana kuhusiana na madeni ya vyama vya ushirika, hali ambayo ilisababisha
wakulima kimsingi kubebeshwa madeni ambayo kwa kiasi kikubwa hata matumizi ya fedha ambazo zimekopwa utaratibu wake haufahamiki sawasawa. Kwa hiyo, hatua ambazo zinachukuliwa ni ili kuondoa hiyo hali, ni ili ifahamike kwamba, mikopo ambayo inachukuliwa inafanya kazi gani, lakini vilevile ni kuwawajibisha wale ambao wamekopa fedha na kuzitumia kwa njia ambazo ni kinyume na taratibu.