Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Abdulla Ally Saleh

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Malindi

Primary Question

MHE. ALLY SALEH ALLY Aliuliza:- Tanzania imekuwa ikipeleka vikosi vya kulinda amani ndani ya Afrika na sehemu nyingine duniani kadri mahitaji na hali inavyoruhusu na kutimiza dhima ya duniani. (a) Je, mazoezi kama haya yanaimarisha jina la Tanzania kiasi gani katika jukumu hili? (b) Kama miaka kumi iliyopita Tanzania imepeleka vikosi maeneo gani na kwa misingi gani? (c) Changamoto gani zinakuwepo katika kukusanya vikosi hivyo kabla havijapelekwa nje ya nchi kwa kzi kama hizo?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Wanaokwenda kwenye maeneo hayo ambako ni kwa kulinda amani mara nyingi hukutana na kujeruhiwa au kufariki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na hapa Tanzania
tumeshuhudia wanajeshi hao wakirudi wakiwa wamefariki na wengine wakijeruhiwa. Je, Serikali, hasa kwenye watu waliofariki, ina utaratibu gani ambao unafanya familia za wanajeshi hao, wapiganaji haokuendelea na maisha baada
ya bread winner wao kufariki? Hilo la kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, Mheshimiwa
Waziri umezungumza hapa kuna matatizo wakati wa kutayarisha vikosi, lakini mimi naona hii ni fursa.
Je, Serikali haioni kwamba, kuna haja ya kujifunza na kutafuta utaalamu kutoka nchi ambazo zime-specialize katika masuala ya kulinda amani, ili iwe ni fursa ya kufungua kituo (centre) ya ku-train watu kwa ajili ya kulinda amani kwa
ajili ya eneo hili la Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika? Ahsante.

Name

Dr. Hussein Ali Mwinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwahani

Answer

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba katika baadhi ya maeneo ya ulinzi wa amani huwa vinatokea vifo na pengine pia huwa watu wanajeruhiwa, lakini upo utaratibu madhubuti
wa kuwafidia kwa yote mawili. Nitoe tu taarifa kwamba kwa wale ambao wamepoteza maisha katika ulinzi wa amani Umoja wa Mataifa wenyewe unafidia na wanaporudishwa hapa familia zao zinapata maslahi yao yote kwa mujibu wa utumishi ambao mhusika alikuwa ameutekeleza hapa nchini.
Kwa hiyo, katika hili hakuna mgogoro, fidia huwa
zinatolewa kama utaratibu unavyotaka kwa wote
waliojeruhiwa pamoja na wale waliopoteza maisha kwa pande zote mbili, Umoja wa Mataifa na Serikali na Jeshi la Wananachi wa Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kujifunza kutoka maeneo mengine juu ya ulinzi wa amani; nataka nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba, hapa Tanzania tunacho chuo cha ulinzi wa amani. Tumepata msaada kutoka kwa Serikali ya Canada, wamekijenga na mara nyingi tunatoa mafunzo, si kwa Watanzania peke yao, ikiwemo na nchi nyingine za Afrika Mashariki wanakuja hapa kujifunza mafunzo haya ya ulinzi wa amani kwa hiyo, hili halina tatizo, tunaendelea vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu langu la msingi, nililosema ni upungufu wa fedha za matayarisho, si suala la mafunzo, mafunzo yapo na chuo tunacho na mafunzo yanaendelea pale kama kawaida.