Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Lucia Ursula Michael Mlowe

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUCIA M. MLOWE aliuliza:- Kilimo cha viazi katika Mkoa wa Njombe kimekuwa ni ukombozi kwa wananchi wa mkoa huo. Zao hilo ni la biashara lakini wananchi wameanza kukata tamaa kutokana na kupanda kwa bei za pembejeo, pembejeo kutokufika kwa wakati na kukosa soko la uhakika:- Je, Serikali ipo tayari kuwaunganisha wakulima hao na kuwa na chama chao kitakachoweza kupigania haki za wakulima hao?

Supplementary Question 1

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza:-
Swali la kwanza, kwa kuwa tatizo la pembejeo
limekuwa la muda mrefu na ni sugu katika Mkoa wetu wa Njombe. Je, Serikali iko tayari sasa kuanzisha Kiwanda cha kutengenezea mbolea katika Mkoa wa Njombe?
Swali la pili, kwa kuwa Mkoa wa Njombe ni kati ya
Mikoa inayotoa viazi au inayolima viazi kwa wingi; Njombe peke yake inalima au inatoa viazi tani 900,000 kwa mwaka, lakini tatizo ni kwamba soko limeingiliwa na watu wa Kenya.
Je, Serikali iko tayari sasa kuwazuia watu wa Kenya wasilete viazi nchini Tanzania ili wakulima wetu wa viazi waweze kuwa na soko zuri?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI KILIMO, MIFUGO NA UVUVI:
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Serikali kujenga Kiwanda cha Mbolea Njombe; Serikali ya Awamu ya Tano inahamasisha ujenzi wa uchumi wa viwanda, kwa hiyo, tuko tayari kushirikiana na Mbunge pamoja na wadau wengine wowote ambao wanataka kuanzisha Kiwanda cha Mbolea- Njombe. Vilevile ni lazima niseme kama nilivyosema, tunategemea bei ya pembejeo ishuke kuanzia mwaka unaokuja kwa sababu karibuni tutaanza utaratibu wa kuagiza mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement). Kuhusiana na suala la ushindani wa Wafanyabiashara kutoka Kenya; kimsingi tunabanwa na itifaki za Kikanda kuhusiana na biashara, kwa hiyo ni vigumu moja kwa moja kuwazuia wakulima wa Kenya isipokuwa tunachofanya ni kujenga mazingira ambayo wakulima wetu wanaweza wakazalisha kwa tija ili waweze kushindana na wafanyabiashara wengine kutoka Kenya.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nipende tu
kumweleza Mheshimiwa Mbunge kwamba ushindani siyo mbaya na mara nyingi Wakenya wanapokuja kununua viazi kutoka kwetu ni kwa sababu kuna tofauti kati ya msimu wa viazi kuzalishwa Njombe na Kenya, kwa hiyo tusiogope
ushindani lakini tujizatiti zaidi tuweze kuzalisha kwa tija ili tuweze kushindana.