Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Serikali imeweka kipaumbele kwenye sekta ya kilimo na kuainisha kwamba mazao ya kilimo yatakuwa moja ya malighafi kwenye viwanda nchini:- (a) Je, Serikali imeweka mkazo gani kwenye vyanzo vya kilimo ambavyo ndivyo vitakuwa malighafi na kusababisha uzalishaji ukue? (b) Je, Serikali ina mkakati gani juu ya uhakika wa wakulima wengi zaidi kuingia kwenye kilimo cha umwagiliaji? (c) Je, Serikali imewekeza kwa kiasi gani kwenye zana za kilimo za kisasa kwa wakulima wadogo na hasa wanawake waishio vijijini?

Supplementary Question 1

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika,
nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Kwa kuwa, zana alizozitaja Mheshimiwa Naibu Waziri zinatumiwa zaidi na wanaume na zinarahisisha zaidi kazi kwa
wanaume, hususan, kwenye kaya zenye uwezo. Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa zana ambazo zitamrahisishia mwanamke kulima mwenye kipato duni kama ninavyomwona mwanamke aishiye Mkoa wa Simiyu? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Ilani ya Chama cha Mapinduzi imekusudia kutoa ajira zaidi. Kwa kupitia malighafi za mazao, si tu ajira zitatoka katika viwanda bali pia katika mazao ambayo yatauzwa na wakulima. Je, Serikali
ina mkakati gani wa kuhakikisha inatoa mbegu ambazo zitaleta tija katika kilimo cha mtama na alizeti katika Mkoa wa Simiyu?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI:
Mheshimiwa Spika, jitihada mbalimbali ambazo Serikali inachukua kuboresha kilimo za kugawa na kuleta zana za kilimo zinawasaidia wakulima wote wakiwemo na wanawake. Tunaamini kwamba tukiweza kuwa na zana za kilimo za kisasa, wanufaika wa kwanza watakuwa ni wanawake kwa sababu wao hasa ndio kwa kiasi kikubwa
wanajihusisha na kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini vilevile Wizara kupitia Mfuko wa Pembejeo imeweka utaratibu wa kuweza kukopesha zana za kilimo kwa bei nafuu na wanawake kwa kupitia vyama vya ushirika lakini vikundi mbalimbali ni wanufaika wakubwa wa huduma hii. Vilevile Wizara kwa kupitia Benki
ya Maendeleo ya Kilimo inatoa mikopo kwa ajili ya pembejeo. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge aweze kuwasiliana na sisi ili kuwaunganisha akinamama wakulima
wa Simiyu ili waweze kupata huduma hii.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kugawa mbegu za mtama na alizeti, katika mwaka wa fedha unaokwisha na hasa baada ya changamoto ya mvua kutokuwa nzuri, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iligawa zaidi ya mbegu milioni 14 za mtama. Vilevile tumegawa mbegu za alizeti kwa wakulima mbalimbali nchini wakiwepo na wakulima wa Mkoa wa Simiyu.

Name

Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Serikali imeweka kipaumbele kwenye sekta ya kilimo na kuainisha kwamba mazao ya kilimo yatakuwa moja ya malighafi kwenye viwanda nchini:- (a) Je, Serikali imeweka mkazo gani kwenye vyanzo vya kilimo ambavyo ndivyo vitakuwa malighafi na kusababisha uzalishaji ukue? (b) Je, Serikali ina mkakati gani juu ya uhakika wa wakulima wengi zaidi kuingia kwenye kilimo cha umwagiliaji? (c) Je, Serikali imewekeza kwa kiasi gani kwenye zana za kilimo za kisasa kwa wakulima wadogo na hasa wanawake waishio vijijini?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwa kuwa matatizo yaliyopo Simiyu yanafanana sana na matatizo yaliyopo Mkoa wa Geita na Kagera, Serikali imetangaza wafugaji watoke kwenye Pori la
Kimisi na Burigi na wakatii sheria. Sasa wale askari wanaoendesha ile operesheni wanazifuata ng’ombe vijijini kilometa saba mpaka kumi na kuzirudisha porini na baadaye kuwafilisi wananchi hawa. Je, ni nini kauli ya Waziri kuhusiana
na uonevu unaoendelea kule Burigi na Kimisi?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO NA UMWAGILIAJI:
Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyoeleza kwamba tayari katika zoezi linaloendelea la kuondoa mifugo katika misitu na hifadhi kuna changamoto ambazo zimeripotiwa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara imepokea changamoto hizo na inaendelea kujadiliana ndani ya Serikali kuangalia namna ya kuzitatua kwa muda mfupi.