Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tauhida Cassian Gallos Nyimbo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS NYIMBO aliuliza:- Kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu yanayotolewa na wachongaji wa vinyago hasa pale wanunuzi wa vinyago hivyo kutoka nje wanaponyang’anywa bidhaa hiyo wafikapo airport kwa madai mbalimbali ikiwemo kutolipa kodi. (a) Je, vinyago hivyo ambavyo ni biashara ya wanyonge baada ya kuzuiliwa hupelekwa wapi? (b) Je, Serikali haioni kuwa kwa kufanya hivyo kunawapotezea wateja na soko kwa wanaofanya ujasiriamali wa aina hiyo lakini pia kuwaingizia hasara?

Supplementary Question 1

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS NYIMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia fursa hii ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza pamoja na majibu aliyonipa Mheshimiwa Waziri lakini sikuridhika na majibu haya.
Mheshimiwa Waziri katika majibu yake ya msingi anasema kwamba kati ya bidhaa ambazo hazitozwi kodi pamoja na vinyago, lakini katika swali hilo hilo la msingi anabainisha kwamba kati ya vitu vinavyokamatwa na kupigwa mnada ni pamoja na vinyago. Mheshimiwa Waziri katika suala hili ulivyolijibu huoni kwamba umejichanganya? Kama vinakamatwa na kupigwa moto, vinakamatwa kwa kosa lipi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia kuuliza swali la pili, je, Serikali imetoa elimu yoyote kuhusiana na suala zima la uuzaji wa vinyago kwa wajasiriamali wadogo wadogo ukizingatia Mheshimiwa Rais ameondosha kodi ndogo ndogo kwa wajasiriamali?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, naomba nikiri kwamba sijamchanganya, vinyago tunafahamu ni bidhaa zinazotokana na maliasili za nchi yetu hivyo inawezekana watu wa Wizara ya Maliasili wanatozo zao ambazo wanazitoza. Mimi nimekanusha utozaji wa kodi ambao tunatoza sisi kama Wizara ya Fedha kwamba hizi hazipo katika orodha ya bidhaa tunazozitoza kodi (extport duty). Kwa hiyo, ndiyo maana katika jibu langu la sehemu ya pili nilisema yawezekana zilikuwa zinatakiwa kulipiwa tozo mbalimbali kutoka katika Wizara ya Maliasili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, elimu ya ujasiriamali tunaendelea kuitoa, kuna kitengo ndani ya Wizara yangu ya Fedha na tunaendela kuifanyia kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wajasirimali wote nchini wakiwepo wafanyabiashara wa vinyago.