Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Peter Joseph Serukamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kaskazini

Primary Question

MHE.PETER J. SERUKAMBA (K.n.y MHE. ZAINAB A. KATIMBA) aliuliza:- Mwaka 1993 Serikali ilianzisha Mfuko wa Maendeleo wa Vijana (Youth Development Fund – YDF) ili kutoa mikopo kwa vijana nchini. Mwaka 2013/2014 Serikali ilitenga jumla ya shilingi bilioni 6.1 na mpaka mwezi Machi, 2014 jumla ya shilingi bilioni mbili zilitolewa na Serikali. (a) Je, Serikali itakuwa tayari kuwaeleza vijana nchi nzima kuwa ni vijana wangapi na wa maeneo gani ambao wamenufaika? (b) Je, maisha ya vijana waliopewa fedha hizo yamebadilika kwa kiasi gani ili tuweze kupima haja ya mfumo huo na usimamizi wake? (c) Je, Serikali haioni ni wakati muafaka sasa kuangalia upya mfumo uendeshaji wa mfuko huo?

Supplementary Question 1

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majawabu mazuri ya Naibu Waziri anaweza sasa leo akawaelekeza Halmashauri zote nchini kwamba kila mwaka ni mandatory lazima kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Vijana?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utaratibu wa kuwasaidia vijana kupata mitaji na mikopo, tunayo mifuko mingi sana. Moja wa mfuko ambao nimeusema hapa ni Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao umekuwa ukishirikiana na Halmashauri kupitia SACCOS mbalimbali na vijana wengi wamekuwa wakipata mikopo kupitia katika SACCOS hizo.
Kwa hiyo, nimuondoe tu hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba kupitia Mfuko huo wa Maendeleo ya Vijana, kila mwaka tumekuwa tukikopesha vijana na wengi wamefaidika kama nilivyosema hapa isipokuwa tu katika zile asilimia tano za kila Halmashauri ambazo ni utaratibu mwingine tofauti, nako tumekuwa tukitoa msisitizo mkubwa kuhakikisha kwamba Halmashauri zinatenga asilimia tano za mapato yao ya ndani kwa ajili ya vikundi vya vijana.

Name

Hamidu Hassan Bobali

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mchinga

Primary Question

MHE.PETER J. SERUKAMBA (K.n.y MHE. ZAINAB A. KATIMBA) aliuliza:- Mwaka 1993 Serikali ilianzisha Mfuko wa Maendeleo wa Vijana (Youth Development Fund – YDF) ili kutoa mikopo kwa vijana nchini. Mwaka 2013/2014 Serikali ilitenga jumla ya shilingi bilioni 6.1 na mpaka mwezi Machi, 2014 jumla ya shilingi bilioni mbili zilitolewa na Serikali. (a) Je, Serikali itakuwa tayari kuwaeleza vijana nchi nzima kuwa ni vijana wangapi na wa maeneo gani ambao wamenufaika? (b) Je, maisha ya vijana waliopewa fedha hizo yamebadilika kwa kiasi gani ili tuweze kupima haja ya mfumo huo na usimamizi wake? (c) Je, Serikali haioni ni wakati muafaka sasa kuangalia upya mfumo uendeshaji wa mfuko huo?

Supplementary Question 2

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti swali la msingi, Mheshimiwa Mbunge aliyeuliza alizungumzia fedha iliyotengwa mwaka 2013/2014 na kiwango ambacho Serikali walikuwa wamekitoa. Nataka kujua ni kiasi gani cha pesa kilitengwa na kimepelekwa katika mwaka huu wa fedha tulionao wa 2016/2017?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, labda kabla sijaenda katika kujibu swali lake nisaidie kutoa ufafanuzi kidogo ili jambo hili lieleweke vyema.
Katika utaratibu wa kuwasaidia vijana nchini iko mifuko mingi ambayo inashughulika na shughuli hii ya kuwasaidia vijana, lakini ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira tunao Mfuko wa Maendeleo wa Vijana ambao pamoja na mfuko huu tunao pia utaratibu wa utengaji wa asilimia tano za mapato ya ndani ya kila Halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ndani ya mfuko wetu mpaka hivi sasa ninavyosema tayari tumeshakopesha vikundi vya vijana takribani 309 na wamepatiwa takribani shilingi 1,700,000,000 kwa hiyo, katika utaratibu ulioko hivi sasa, mwaka huu wa fedha tumetengewa shilingi bilioni moja ambako hizo nazo tutazisambaza kwa ajili ya vikundi vya vijana ili waweze kunufaika Nchi nzima.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri naomba kuongeza tu hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala zima la Halmashauri mwaka huu katika Bajeti ya Halmashauri kwanza tulitoa maelekezo katika utengenezaji wa Bajeti ya mwaka 2016/2017 ni lazima kila Halmashauri itenge 10% ya tano kwa vijana na tano kwa akina mama ambapo jumla ya fedha zote shilingi bilioni 64.5. Katika fedha hizo sasa kwa hivi sasa katika upande wa Halmashauri tumeenda sasa hivi karibuni shilingi bilioni tano Halmashauri mbalimbali zimeshaanza kutoa hivi sasa niwaelekeze Halmashauri mbalimbali sasa suala lile siyo suala la hiari, ni suala la lazima kila Halmashauri lazima itoe asilimia tano kwa vijana na asilimia tano kwa akina mama na hata hivyo mchakato wa bajeti tunaoondoka nao hivi sasa Halmashauri yoyote tutaizuia bajeti yake mchakato wake mpaka ile commitment tuloiwekea iwe imetekelezeka katika mwaka huu wa fedha.