Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Suzana Chogisasi Mgonukulima

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUZANA C. MGONUKULIMA aliuliza:- Miradi mingi ya maendeleo inashindwa kumalizika kwa wakati kutokana na Serikali Kuu kutokuleta fedha za miradi kwa wakati:- Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa wakati kwenye Halmashauri ili miradi ya maendeleo itekelezwe kwa kipindi kilichopangwa?

Supplementary Question 1

MHE. SUZANA C. MGONUKULIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na
majibu ya Waziri, Manispaa ya Iringa ina miradi mikubwa ya Machinjio ya Kisasa
ya Ngelewala, Soko la Ngome, Sekondari ya Mivinjeni, Nyumba za Waganga na
Wauguzi wa Zahanati ya Njiapanda na Nduli. Katika Baraza la Madiwani, kupitia
bajeti ya mwaka 2016/2017, Manispaa ya Iringa ilikadiria kukusanya mapato ya
ndani Sh. 4,532,000,000 ili kuweza kumalizia miradi midogo iliyokuwa inaikabili
Manispaa hiyo. Manispaa ya Iringa, vyanzo vikuu vya mapato vinatokana na
kodi ya majengo, Serikali ikaamua kodi hizi za majengo zikusanywe na TRA, je, ni
lini Serikali itaona umuhimu wa kupeleka hela za miradi hii kwa wakati ili kuweza
kumalizia miradi ambayo haijamalizika hadi sasa?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika,
napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba Serikali inaona umuhimu wa
miradi yote ya maendeleo kama ilivyopitishwa katika bajeti yetu mwezi Juni.
Hivyo, kama nilivyosema katika jibu langu la msingi, kinachopelekea kupeleka
fedha hizi ni upatikanaji wa fedha hizi. Kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge
ameongelea kuhusu kodi ya majengo, naomba nimwambie kwamba TRA
imekusanya kodi ya majengo mwezi wa Kumi, baada ya quarter ya kwanza
kupewa Halmashauri zenyewe kukusanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge,
anapuhudhuria Baraza la Madiwani aweze kusimamia mapato yaliyopatikana ili yaweze kutumika katika miradi aliyoitaja. Serikali yetu baada ya kukusanya
kuanzia mwezi wa Kumi, fedha zote tulizoahidi zitarejeshwa katika Halmashauri
husika kutokana na bajeti zilizopitishwa.