Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Kumekuwa na mgogoro kati ya wafugaji na wakulima wa Jimbo la Same Mashariki dhidi ya TANAPA:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwapatia wafugaji hao shamba darasa kupitia hekta 346,000 zinazofaa kwa ufugaji? (b) Ili kutatua tatizo la maji na malisho kwa wafugaji wa Same Mashariki: Je, Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi haioni umuhimu wa kuanzisha mradi wa kuvuna maji ya mvua ambazo hunyesha mara kwa mara? (c) Je, Waziri yuko yatari kuambatana na wataalam wake kutembelea Jimbo la Same Mashariki ili kuona ni jinsi gani anaweza kuwasaidia wafugaji kuanzisha mitambo ya Biogas kwenye mazizi yao pamoja na kuwaelimisha matumizi bora ya mbolea ya samadi?

Supplementary Question 1

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Kabla ya swali langu la nyongeza, nataka nieleze masikitiko yangu makubwa
kwa jinsi aliyempa Mheshimiwa Waziri taarifa hii alivyoipotosha. Mheshimiwa
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi namheshimu sana na inabidi kueleza
ukweli kwamba upotoshaji huu, itabidi huyu aliyempa hizi taarifa za uwongo amchukulie hatua. Kwa mfano, hapa ilipoandikwa kwamba, TANAPA
wakishirikiana na WOYOGE Trust Fund wameshajenga birika ni uwongo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza na-declare interest, hii WOYOGETrust
fund mimi ndiyo Mwenyekiti wake. Huu mradi mwaka jana nilimuuliza Waziri wa
Maliasili na Utalii, kwamba wanyama wale wameharibu sana miundombinu
ambayo nilikuwa nimewasaidia wananchi kule kwa ufadhili wa Ubalozi wa Japan
na Waziri akakubali kwamba watarekebisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, basi
nimwambie tu kwamba, Waziri amepotoshwa maana TANAPA hawajaja kujenga
chochote kwanza ndiyo naambiwa mradi umeenda kwenye Bodi na kwamba
hata haujapitishwa. Wamempotosha sana.
Swali langu la nyongeza ni kwamba je, Waziri haoni kuna umuhimu wa
kuweka kituo cha artificial insemination, kwa kuzingatia kwamba madume
yanayopelekwa kusaidia wafugaji yanakufa, maana wafugaji wanayaswaga
nayo yale yanataka yafanyiwe zerograzing? Naomba ajibu swali hilo.

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika,
kuhusu taarifa tulizotoa kupishana na taarifa aliyonayo yeye, niko tayari kukaa
naye kuangalia kwa nini yeye ana taarifa tofauti na ile ambayo tunayo kama
Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu artificial insemination ningependa
kumjulisha Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari huduma za artificial insemination
zinatolewa karibu kabisa na Jimboni kwake akifika tu kituo cha Tengeru, huduma
hizi zinaweza kupatikana vilevile niko tayari kukaa naye na kumwelekeza zaidi
namna ya wafugaji wake watakavyoweza kunufaika na huduma hii.

Name

Yussuf Salim Hussein

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Chambani

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Kumekuwa na mgogoro kati ya wafugaji na wakulima wa Jimbo la Same Mashariki dhidi ya TANAPA:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwapatia wafugaji hao shamba darasa kupitia hekta 346,000 zinazofaa kwa ufugaji? (b) Ili kutatua tatizo la maji na malisho kwa wafugaji wa Same Mashariki: Je, Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi haioni umuhimu wa kuanzisha mradi wa kuvuna maji ya mvua ambazo hunyesha mara kwa mara? (c) Je, Waziri yuko yatari kuambatana na wataalam wake kutembelea Jimbo la Same Mashariki ili kuona ni jinsi gani anaweza kuwasaidia wafugaji kuanzisha mitambo ya Biogas kwenye mazizi yao pamoja na kuwaelimisha matumizi bora ya mbolea ya samadi?

Supplementary Question 2

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa
kunipa nafasi. Jimbo la Same Mashariki ni Jimbo ambalo lina ardhi nzuri kwa
kilimo cha tangawizi: Je, Mheshimiwa Waziri kwa nini huoni sababu wataalam
wake kushirikiana na wataalam wa TANAPA kuwapa elimu wananchi wa eneo
hili wakalima kilimo cha tangawizi ambacho hakidhuriwi na mifugo,
tukaondokana na mzozo wa wakulima na wafugaji?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni
kweli kabisa kama alivyosema kwamba eneo la Same kutokana na hali ya hewa na aina ya udongo inafaa sana kwa zao la tangawizi, tayari Wakulima wa Same
ni wakulima mahiri wa zao la tangawizi, na tayari Serikali kwa kushirikiana kwa
karibu sana na aliyekuwa Mbunge wa Same Mheshimiwa Anne Kilango
Malecela, ambaye tunashukuru amerudi kwenye Bunge hili walishajenga
kiwanda kwa ajili ya kuchakata tangawizi kama njia ya kuwaongezea wakulima
faida zaidi.