Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

John John Mnyika

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Kibamba

Primary Question

MHE. JOHN J. MNYIKA aliuliza:- Wananchi wa Mloganzila waliopisha ujenzi wa MUHAS hawakulipwa fidia ya ardhi au angalau “mkono wa kwaheri” na wapo wenye madai ya „kupunjwa‟ fidia ya maendelezo:- (a) Je, ni lini wananchi hao watapewa malipo yao kama Serikali ilivyoahidi? (b) Je, ni kwa namna gani Serikali imeshughulikia madai ya mapunjo ya fidia ya maendeleo?

Supplementary Question 1

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kwanza Mheshimiwa Naibu Waziri katika sehemu (a) ya swali hajajibu swali. Niliuliza ni lini hii fidia ya hisani italipwa lakini hajajibu ni lini na Mheshimiwa Lukuvi, Waziri wa Ardhi anafahamu kwamba jambo hili ni la muda mrefu. Mwaka 2009 aliyekuwa Waziri wa Ardhi wakati huo Chiligati aliahidi wangelipwa milioni tisa, hawakulipwa mpaka mwaka 2015 wananchi wakaandamana kwenda Wizarani, Serikali ikaahidi kulipa milioni mbili badala ya ile milioni tisa. Sasa sehemu (a) ni vyema Waziri akajibu ni lini hasa Serikali italipa hii fidia. Au inataka sasa kwa kuwa wakati ule tuliandamana kwenda Wizara ya Ardhi sasa tuandamane kwenda kwa Mheshimiwa Magufuli ajibu ni lini hasa hii fidia italipwa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sehemu (b) ya swali. Serikali imesema kwamba haidaiwi mapunjo ya fidia ya maendelezo. Hili jibu la Serikali ni jibu la uongo. Mwezi Aprili mwaka 2014 tulikuwa pamoja na Rais Dkt. Jakaya Kikwete pale Mloganzila, jambo hili likajitokeza na Rais akataka vielelezo tukamkabidhi na sio Rais tu, Wizarani kuna nakala za fomu za watu ambao kimsingi walipunjwa fidia za maendelezo kinyume kabisa na thamani halisi ya mali zilizokuwepo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa sababu Serikali imejibu uongo hapa Bungeni; je, Serikali iko tayari kurudi kwenda kuchunguza malalamiko ambayo yako tayari Wizarani? Vielelezo vyote viko Wizarani na ikalipa fidia ya maendelezo pamoja na kujibu maswali kwa ukweli?

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nilijibu swali lake (a) analosema kwamba sikulijibu. Nadhani katika majibu ya awali nilipojibu sehemu (a) na (b) nimesema kwamba watalipwa baada ya kupatikana fedha na hii haijalipwa kutokana na ufinyu wa pesa sasa siwezi kuweka commitment ya Serikali hapa wakati natambua wazi kwamba haya mambo yanakwenda kwa bajeti kama halipo katika bajeti siwezi kukwambia ni kesho tutalipa au kesho kutwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo nilitaka kutoa ufafanuzi huo. Kwa sababu ukisema unaweka commitment leo na pesa haijapatikana, atakuja kusema baadaye kwamba tumedanganya Bunge na sisi hatutaki kulidanganya Bunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika majibu yangu pia hakuna mahali ambapo tumedanganya Bunge. Kwanza kwa sababu hata hao unaowasema wamekuwa wakija sana ofisini wakidai madai yao na tunawaambia nini kilikwisha fanyika na mpaka sasa kitu gani ambacho wanadai. Lakini ukiangalia pale hakuna mapunjo ambayo wanatakiwa walipwe isipokuwa ile iliyosemwa ya hisani ambayo tunasema watakuja kulipwa baada ya kupatikana ndiyo hiyo ambayo Serikali inaifanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hatuwezi kusema kwamba kuna watu walipunjwa na ukizingatia kwamba eneo lile ambalo watu wanalipigia kelele bado ilikuwa ni sehemu ya Serikali. Ilikuwa ni viwanja vya Serikali isipokuwa kulikuwa na vijiji vilivyokuwa vinatambulika mle na ndiyo maana Serikali ikawa tayari kulipa fidia ya maendelezo katika yale maeneo waliyokuwa nayo.