Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Shukuru Jumanne Kawambwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA aliuliza:- Kumekuwa na tatizo la muda mrefu la ukosefu wa maji safi na salama katika Mji Mkongwe wa Bagamoyo katika Kata za Magomeni na Dunda:- Je, ni lini Serikali itawapatia wananchi wa Mji Mkongwe Bagamoyo maji kwa kiwango cha kuridhisha?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Moja, kwa vile Waziri amekiri kwamba maji yanapatikana kwa mgao: Je, Waziri atakuwa tayari kuiagiza DAWASCO ili iiondoe hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo katika utaratibu wa mgao ili kuweza kuboresha huduma ya afya katika hospitali hii ya Wilaya?
Swali la pili; je, mradi huo wa usambazaji mabomba utajumuisha kata zote tisa za Mamlaka ya Mji Mdogo wa Bagamoyo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Shukuru Kawambwa nikuhakikishie, baada ya mradi huu kukamilika mwezi Juni, 2017 Hospitali ya Bagamoyo haitakuwa na matatizo ya maji tena. Katika Mkataba unaoendelea, suala hili limeainishwa kuhakikisha kwamba Hospitali ya Bagamoyo isiwe na matatizo ya maji tena.
Swali la pili; mpango huu ukikamilika Mheshimiwa Kawambwa ni kwamba Kata zote tisa za Jimbo lako Bagamoyo zitapata huduma ya maji kutokana na mradi huu.