Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:- Serikali inatakiwa kuweka mkakati wa kuhakikisha mazao yanauzwa katika vituo maalum vinavyotambuliwa ili kuzuia walanguzi kufuata mazao shambani na kununua kwa bei ndogo:- Je, Serikali haioni kuwa kuna umuhimu wa kutunga sheria kuzuia walanguzi kwenda kununua mazao shambani?

Supplementary Question 1

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Serikali imekiri kwamba kuna umuhimu wa kuwa na sheria hii na pia imesema imetunga sheria kwa ajili ya mazao yale yanayosimamiwa na bodi ya mazao: Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuweza kufanya marekebisho katika sheria hiyo ili hata mazao mengine mchanganyiko yaweze kulindwa ili wakulima waweze kufanikiwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; ni wazi kwamba bado ulanguzi wa mazao unaendelea, walanguzi wanafuata wakulima mashambani na siyo sahihi kusema kwamba magulio ni sehemu ya ushindani wa bei na Halmashauri zenyewe hazijawa na mkakati maalum wa kuweza kuunda sehemu za kuuzia mazao na kuweza kuzisimamia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali inachukua hatua zipi kuhakikisha kwamba vituo hivi vinakuwepo na vinakuwa na usimamizi ili wakulima waweze kunufaika kwa kupata bei nzuri kuweza kubadilisha maisha yao?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

Mwenyekiti, ni kama ambavyo nimeeeleza katika jibu la swali la msingi kwamba Serikali inaona umuhimu wa kuanzisha sheria.
Kwa hiyo, ombi lake tumelipokea na Serikali imeshaonesha nia kwamba hilo inalishughulikia na imeshaanza kufanya kwa mazao hayo mengine. Kwa maana nyingine tutaendelea kushughulikia na mazao mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kule kwetu Namtumbo magulio kwa kweli huwa yanaleta ushindani. Kwa hiyo, naungana kabisa na jibu la msingi kwamba Halmashauri waimarishe magulio na sehemu za minada kwa kweli maeneo hayo yanaleta ushindani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna njia nyingine kutokana na mazao mbalimbali mengine, tuwasiliane na Halmashauri hizo na sisi ni wajumbe wa Halmashauri, tuweze kuboresha kanuni zetu, bylaws zetu, ili tuhakikishe mkulima anapata haki yake kwa jasho analolitoa.