Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jaku Hashim Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Kumekuwa na malalamiko ya wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania ambao ni wazawa kulipishwa ada ya masomo yao kwa fedha za kigeni badala ya fedha za Kitanzania wakati wao ni Watanzania na vyuo hivyo viko hapa nchini licha ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kulipigia kelele sana jambo hilo:- (a) Je, Serikali inatambua kuwa kuna tatizo hili na kama inatambua imechukua hatua gani dhidi ya tatizo hilo? (b) Kwa kuwa kilio hiki kipo kwenye taasisi mbalimbali kama vile bandarini, uwanja wa ndege, hoteli na taasisi za fedha na kadhalika, je, Serikali inatoa tamko gani juu ya jambo hili? (c) Je, kuna sheria yoyote ya nchi inayomtaka mwanachuo wa Kitanzania kulipa ada kwa pesa ya kigeni?

Supplementary Question 1

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na kutotaka kuniona naomba niulize maswali madogo sana mawili ya nyongeza na niombe Waziri wa Fedha awe tayari kumsaidia Naibu Waziri. Ninachozungumza ni Kiswahili wala si Kihindi. Waziri wa Fedha ningeomba akainuka yeye maana hili swali linamhusu yeye. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge ni chombo kizito cha Tanzania na Watanzania wametutuma ili tuyasemee matatizo yao. Mheshimiwa Naibu Waziri au Waziri atakuwa yuko tayari kujiuzulu pindi nikimletea ushahidi wa kutosha juu ya suala hili? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia tena, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kujiuzulu pindi nikimletea ushahidi wa kutosha juu ya kadhia hii kwa vijana wa Tanzania kutozwa fedha za kigeni katika vyuo hivyo na anajibu hapa hamna? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, je, amefanya utafiti kwenye vyuo gani mpaka akatueleza hakuna utaratibu wa kutoza fedha za kigeni ili Bunge lako liweze kuridhia tatizo hili? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, swali la tatu, hakuna sheria…

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu yeyote anayekuwa hatendewi haki kwa mujibu wa sheria anayo fursa ya kuchukua hatua. Hatua mojawapo ni pamoja na kutoa taarifa kwa ngazi zinazohusika. Ndiyo maana nimesema kwamba kwa kipindi chote hiki Wizara yetu haijaweza kupata taarifa na hata wewe ulivyoendelea kuuliza umeshindwa hata kutuambia mfano wa chuo ambacho kinafanya hivyo. Kwa misingi hiyo, mimi nachukulia hilo suala halipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuhusiana na kufanya utafiti, ni sawa, ni jambo jema, hilo nalichukua kuendelea kulifanyia kazi.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali hili limekuwa likijirudia mara nyingi na naomba nitoe maelezo kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Kigeni ya mwaka 1992 inamruhusu mtu yeyote kupokea na kumiliki na kutumia fedha za kigeni kwa shughuli za kiuchumi. Kwa hiyo, hao wenye shule siyo kwamba hawaruhusiwi, hilo la kwanza tuelewane.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 inaweka bayana kabisa kwamba legal tender ya nchi yetu ni Shilingi ya Kitanzania. Nilikwishalieleza Bunge lako Tukufu kwamba ni makosa kwa mtu yeyote kukataa Shilingi ya Tanzania kwa malipo hapa nchini. Kwa hiyo, narudia tena, pale ambapo kuna Mtanzania yeyote anakwenda kulipa ada au malipo mengine akadaiwa kwa dola lakini yeye akatoa Shilingi za Kitanzania akakataliwa, atoe taarifa mara moja ili tuchukue hatua za kisheria. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine Benki Kuu tumeshafanya utafiti na nilikwishalitolea taarifa hapa ni 3% tu ya shughuli mbalimbali ambazo wana-quote bei zao kwa dola. Kwa hiyo, kosa ni kukataa shilingi kosa sio ku-quote bei zao kwa dola.

Name

Ally Abdulla Ally Saleh

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Malindi

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Kumekuwa na malalamiko ya wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania ambao ni wazawa kulipishwa ada ya masomo yao kwa fedha za kigeni badala ya fedha za Kitanzania wakati wao ni Watanzania na vyuo hivyo viko hapa nchini licha ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kulipigia kelele sana jambo hilo:- (a) Je, Serikali inatambua kuwa kuna tatizo hili na kama inatambua imechukua hatua gani dhidi ya tatizo hilo? (b) Kwa kuwa kilio hiki kipo kwenye taasisi mbalimbali kama vile bandarini, uwanja wa ndege, hoteli na taasisi za fedha na kadhalika, je, Serikali inatoa tamko gani juu ya jambo hili? (c) Je, kuna sheria yoyote ya nchi inayomtaka mwanachuo wa Kitanzania kulipa ada kwa pesa ya kigeni?

Supplementary Question 2

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Zama hizi si rahisi kukataa kuja kwa wawekezaji kuwekeza katika shule za kigeni na vyuo vikuu mfano ni Shule za Sekondari kama Feza na nyinginezo. Serikali haioni kuna haja kwa utata huu unaotokezea, kwa mfano Chuo cha KIU, Chuo Kikuu cha Zanzibar kiliwahi kutoza kwa dola na Serikali inasema haijui kuwa na sera ya vyuo au shule zinazokuja hapa ili waelewe nini wafanye na nini wasifanye ikiwa ni pamoja na kutolazimishwa na nchi za kigeni kufunga shule kwa sababu ya maslahi yao? Ahsante.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi vyuo vyote vimeshaelekezwa na vimejua nini wajibu wao kufuatana na kanuni na taratibu na sheria hizi. Labda jambo ambalo naweza nikalichukua ni kuendelea kuvikumbusha vyuo kama ambavyo tumekuwa tukifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutumia nafasi hii niombe tu kuvisisitiza vyuo pamoja na kwamba wanao uhuru huo wa kuweza kutumia fedha za kigeni lakini suala liwe ni kwamba mwananchi wa Tanzania sarafu yake ni Shilingi ya Kitanzania. Kwa hiyo, hiyo ipewe kipaumbele badala ya kutoa kipaumbele kwa fedha za kigeni.