Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jaku Hashim Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB (K.n.y. MHE. IBRAHIMU HASSANALI MOHAMMEDALI) aliuliza:- Wenye maduka waliopewa kibali cha kuegesha magari yao kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni wameonekana wakihodhi nafasi hiyo kwa saa 24:- (a) Je, ni lini watu wenye tabia hiyo watachukuliwa hatua za kisheria? (b) Katika Jiji la Dar es Salaam wakati wa usiku inakuwa kama mji huo hauna sheria kwa sababu wenye magari huegesha magari hovyo na kusababisha adha kwa watu wengine. Je, ni lini Serikali itawachukulia hatua watu wa aina hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nina maswali ya nyongeza, mji umebadilika, je, Serikali haioni haja nayo ibadilike kuleta sheria nyingine?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa baadhi ya watendaji wake wanaokusanya zile shilingi mia moja hamsini, mia mbili wamekuwa na kauli ambazo haziridhishi kwa wananchi, je, anatoa wito gani?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mji umebadilika lakini kama nilivyosema kwamba Halmashauri ya Jiji kuna sheria ambayo inaongoza utaratibu katika maeneo hayo nayo ni Sheria Ndogo yenye GN Na.60. Naamini kwa sababu kuna wadau mbalimbali na Mheshimiwa Jaku najua ni mdau wa Jiji la Dar es Salaam lakini na Wabunge na Waheshimiwa Madiwani wa maeneo hayo kama wakiona kuna haja ya kurekebisha Sheria Ndogo hiyo basi wafanye hivyo na sisi Ofisi ya Rais - TAMISEMI ambao ndiyo wenye jukumu la kufanya mchakato huu uweze kukamilika tutalishikia bango jambo hili liweze kuwa mahali pazuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini suala lingine alilosema ni kuhusu kero ya ukusanyaji wa fedha hizo lakini hata uaminifu wa upelekaji fedha zile haupo. Kwa bahati nzuri sasa hivi katika Jiji la Dar es Salaam tuna Mkurugenzi makini sana naamini kwa hizi changamoto ndogondogo zinazobainika tutazisimamia kwa pamoja ili kuzitatua. Lengo ni wananchi wanaoegesha magari yao katika Jiji lile kupata huduma bora bila kupata usumbufu.

Name

Ally Mohamed Keissy

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB (K.n.y. MHE. IBRAHIMU HASSANALI MOHAMMEDALI) aliuliza:- Wenye maduka waliopewa kibali cha kuegesha magari yao kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni wameonekana wakihodhi nafasi hiyo kwa saa 24:- (a) Je, ni lini watu wenye tabia hiyo watachukuliwa hatua za kisheria? (b) Katika Jiji la Dar es Salaam wakati wa usiku inakuwa kama mji huo hauna sheria kwa sababu wenye magari huegesha magari hovyo na kusababisha adha kwa watu wengine. Je, ni lini Serikali itawachukulia hatua watu wa aina hiyo?

Supplementary Question 2

MHE. ALLY M. KEISSY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Jiji la Dar es Salaam linashangaza kwani wamechukua kampuni ya kutoka Kenya ili kukusanya fedha za maegesho ya magari Dar es Salaam. Vilevile hawatumii mashine za EFD kukusanya pesa na kupandisha kutoka Sh.300 kwenda Sh.500. Hivi kweli nchi nzima ya watu milioni 50 wamekosa kampuni yoyote katika nchi yetu mpaka kuchukua Kampuni ya Kenya?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue concern hii ya Mheshimiwa Keissy lakini ninavyojua katika suala la ukusanyaji Manispaa za Ubungo, Ilala na Kinondoni zinakusanya zenyewe lakini kwa ukubwa wake Manispaa ya Temeke na Kigamboni, Halmashauri ya Jiji yenyewe inasimamia jambo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala la kampuni kutoka Kenya kukusanya nadhani huo ni mchakato wao lakini ninavyojua ni kwamba kuna utaratibu maalum kwa Jiji la Dar es Salaam, kila Manispaa kwa maana ya Ilala, Kinondoni na Ubungo zina utaratibu wake wa kukusanya ila Manispaa ya Temeke na Kigamboni Jiji lenyewe linasimamia kwa taarifa nilizokuwa nazo, wanasimamia kama Wakala wa Jiji la Dar es Salaam. Kwa hiyo, Mheshimiwa Keissy kuhusu hii kampuni kutoka Kenya kukusanya fedha hizi ngoja tuzi-cross check zaidi lakini inawezekana ni taarifa za kimagazeti zaidi kuliko uhalisia wake.